Mwanariadha wa Kenya bingwa wa mita 400 mwaka 2015 Nicholas Bett afariki kwenye ajali ya barabarani

Nicholas Bett akisherehekea ushindi wake kwenye mshindano ya ridha ya Ubingwa wa Dunia mjini Beijing mwaka 2015 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicholas Bett akisherehekea ushindi wake kwenye mshindano ya ridha ya Ubingwa wa Dunia mjini Beijing mwaka 2015

Nicholas Bett, bingwa wa dunia wa mbio za 400m kuruka viunzi wa mwaka 2015, amefariki dunia kwenye ajali ya barabarani iliyotokea eneo la Lesso, jimb la Nandi katika eneo la Bonde la Ufa.

Taarifa zinasema alikuwa safariki kwenda kumtembelea rafiki yake gari lake lilipogonga tuta barabarani na kubingiria mara kadha.

Alikuwa hajamaliza siku mbili tangu arejee kutoka mashindano ya ubingwa wa riadha Afrika mjini Asaba, Nigeria.

Kamanda wa polisi huko Nandi Patrick Wambani alithibitisha kuwa Bett alifariki wakati gari lake lilipoteza njia na kutumbukia kwenye mtaro barabara ya kutoka Lessos kwenda Eldoret.

"Nimezungumza na Milcah (Chemos) ambaye yuko eneo hilo na amethibisha. Ni kisa cha kuhusunisha kwa sababu nilizungumza naye mwendo wa saa tano asubuhi jana. Alikuwa ameenda Nairobi kumuona daktari kutokana na jeraha alilopata Asaba na angekuja AK kupata barua," afisa wa shirikiso la riadha nchini Kenya Barnaba Korir alikiambia kituo cha Capital mjini Nairobi.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicholas Bett (katikati) alishinda dhahabu kwenye mshindano ya ridha ya Ubingwa wa Dunia mjini Beijing mwaka 2015

Bett alijitoa kutoka mashindano wa mita 400 huko Asaba Nigeria kutokana na jeraha katika mbio ambazo ndugu yake Aron Koech ambaye alishinda dhahabu katika mbio za mita 400 kupokezana vijiti alimaliza nafasi ya nne.

Mwanaridha huyo wa miaka 28 alipata umaarufu mwaka 2015 wakati alishinda dhahabu kwenye mshindano ya riadha ya Ubingwa wa Dunia mjini Beijing ambapo Kenya ilichukua nambari moja duniani.

Tangu wakati huo amekuwa akisumbuliwa na majereha lakini alikuwa na matumaini ya kurejea tena mwaka ujao wakati wa mashindano ya dunia ya IAAF World Championship huko Doha Qatar.

Mada zinazohusiana