Mambo muhimu kuhusu watoto wanaofanikiwa kuwa wachezaji soka England: Kwa nini mtoto 'aitwe' Daniel Da Silva

Mtoto

Ligi ya Premia ni nyumbani kwa baadhi ya wachezaji maarufu zaidi duniani, na ni jambo linaonekana kuwa lisilowezekana kufikiri kuwa mtota wako anaweza kuwa miongoni mwa wachezaji kama hao.

Sivyo.

Utafiti umefanyiwa wachezaji 536 kutoka timu 20 zilizokuwa kwenye ligi mwaka 2017-18 kukuwezesha kubaini ikiwa mtoto wako anaweza kufika kileleni mwa ligi ya Uingereza. Kutokana na utafiti huu unaweza kuchukua hatua hizi kumwezesha mtoto kuingia katika taaluma ya soka.

Tahadhari: Kwa kutumia mbinu hizi hatuwezi kuhakikishia kuwa mtoto wako anaweza kuja kuwa mcheza soka hodari

Wakati wa kumzaa mtoto wako

Sasa hili litahitaji kupangwa vizuri na uhakikishe kuwa mtoto wako amezaliwa tarehe 28 Mei ambayo ni siku ya kuzaliwa ya wachezaji wengi wa Ligi ya Premia. Wanasoka watano walikuwa na bahati ya kuzaliwa tarehe hii na kama mtoto wako naye atabahatika itakuwa vyema.

Hii ni kutokana na sababu watatu kati ya wachezaji hawa wako timu moja. Ikimaanisha kuwa mara moja kwa mwaka Phil Foden, John Stones na Kyle Walker watakata keki moja huko Manchester City.

Kwa wale ambao hawawezani na hili basi tarehe 15 ya kila mwezi huzalisha wachezaji bora zaidi, Januari ukiwa mwezi maarufu zaidi huku Jumatano ikiwa ndiyo siku maarufu zaidi ya kuzaliwa kwa wachezaji.

Kwa hivyo hii inakupa njia ya kukakisha mtoto wako ata uwezekano wa juu wa kuwa kwenye ligi ya Uingereza.

Jinsi ya kumvalisha mtoto wako

Ushauri mkuu: Wanunulie nguo kubwa ili wakue nazo. Wachezaji wa ligi ya Premia wana kimo cha wastani cha sentimita 182.9 karibu futi 6.

Haki miliki ya picha iStock
Image caption Jezi nambari 7 ndiyo maarufu zaidi

Lakini kimo sio kila kitu: Wanaweza kuwa wafupi hadi hata sentimita 161 (futi 5) kama Angel Gomes wa Manchester United. Pia unaweza kujaribu kuandika herufi 7 nyuma ya jezi au fulana za mtoto wako kwa kuwa ndio namba huvaliwa sana kwenye Ligi ya Premia.

Sehemu ambapo utamlea mtoto wako

Taarifa nzuri kwa wazazi wote wanaoishi jijini London kwa sababu hawahitaji kuhama. Huu ndio mji umezalisha wachezaji wengi zaidi katika Ligi ya Uingereza ukiwa na asilimia 2.8 ya wachezaji wanaotokea hapa.

Liverpool inachukua asilimia (1.3%), Birmingham (1.3%), Manchester (1.1%) na Sheffield (0.9%), huku asilimia ndogo ikichukuliwa na Bath (0.6%), Chester (0.6%) na Stockport (0.9%)

Pia kuna nchi nje ya Uingereza zinazoonekana kuwa bora kwa kuzalisha wachezaji wa Ligi wa Premia zikiweko Ufaransa, Uholanzi, Ujerumani na Uhispania huku nao mji mku wa Senegal Dakar na mji wa Uholanzi Amsterdam, ikiwa miji maarufu zaidi ya kigeni kuzalisha wachezaji wa Ligi ya Kuu ya England.

Jina unalompa mtoto wako

Mwisho ni majina yapi unaweza kumpa mtoto ili apate kuwa na bahati ya kucheza katika Ligi ya Premia.

Jina maarufu zaidi la kwanza kati Ligi ni Daniel, la kati kati ni James na jina la mwisho ni Silva ambalo mara nyingi huwa na 'da'

Haki miliki ya picha iStock

Majina ya katikati hayana uzito sana kwa sababu wengi wa wachezaji huwa na jina moja tu. Ni wachezaji watano wana majina matatu ya kati kama vile mchezaji wa Brighton David Petrus Wenceslaus Henri Propper..

Kwa ufupi kwa kufuata takwimu hizi, ndipo uweze kuwa na mchezaji kamili unafaa kujifungua mtoto mnamo 28 Mei London na umpe jina Daniel James na Silva, kisha nguo kubwa ziwe tayari umvalishe. Kisha basi, uanze kumfundisha kucheza soka.

Mada zinazohusiana