Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 09.08.2018: Mourinho, Maguire, Vida, Dembele, Drinkwater, Kurzawa

Harry Maguire Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Maguire

Mlinzi wa Leicester na England Harry Maguire bado ana matumaini kuwa anahamia Manchester United ambayo ofa zake mbili tayari zimekataliwa na mchezaji huyo mwenye miaka 25. (Sky Sports)

Nao Leicester wana nia ya kumuuza Maguire kwenda Manchester United. (Daily Mail)

Naye meneja wa Manchester United Jose Mourinho ana wasiwasi klabu hiyo itakosa kumsaini mchezaji yeyote kabla ya siku ya mwisho leo Alhamisi. (Times)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Domagoj Vida

Arsenal wanatathmini hatua za mwisho kumwendea mchezaji raia wa Croatia Domagoj Vida baada ya kuambiwa kuwa watalipa pauni milioni 26.9 kumsaini mchezaji huyo mweye miaka 29 mlinzi wa Besiktas. (London Evening Standard)

Arsenal wanaweza kutumia pauni milioni 10 kwa mkopo wa msimu wote kwa mshambuliaji wa Barcelona mwenye miaka 21 Mfaransa Ousmane Dembele, wakiwa mpango wa kulipa pauni zingine milioni 90 ili mchezaji huyo aweze kuhama kabisa msimu ujao. (Mundo Deportivo, kupitia Football London)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jerome Boateng

Manchester United wamemkosa mlinzi wa Bayern Muninch raia wa Ujerumani mwenye miaka 29 Jerome Boateng kwa sababu walikuwa wanamtaka kwa mkopo tu. (Sun)

Boateng amekubali kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain, huku Bayern wakijiandaa kumuuza kwa pauni milioni 40.5. (Le Parisien)

Mchezaji mwenye umri wa miaka 22 wa Aston Villa na kiungo wa kati wa England Jack Grealish hajakata tamaa ya kujiunga na Tottenham kabla ya tarehe ya mwisho, licha ya klabu yake kuzuia kuhama kwake kwa gharama ya pauni milioni 25. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kurt Zouma

Everton na Manchester United wako makini kumsaini beki wa Chelsea mwenye miaka 23 Mfaransa Kurt Zouma. (L'Equipe)

Leicester wanafikiri kumrejesha kiungo wa kati wa England Danny Drinkwater kutoka Chelsea, mwaka mmoja baada ya kumuuza kiungo wa kati mwenye miaka 28 kwa pauni milioni 35. (Independent)

West Ham na Cystal Palace pia wanamwinda Drinkwater. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Drinkwater

Everton wanajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Ureno Andre Gomes. (Daily Mail)

Wolves wanajiandaa kumsaini beki wa Manchesetr City raia wa Ukrain mwenye miaka 21 Oleksandr Zinchenko. (Guardian)

Wolves pia wanamtaka beki wa Paris St-Germain Mfaransa mwenye miaka 25 Layvin Kurzawa. (Sun)

Newcastle wanakaribia kumsaini mlinzi wa Barcelona Mbrazil mwenye miaka 22 Marlon Santos kwa mkopo wa msimu mmoja. (Sport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Islam Slimani

Mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani anavutia vilabu vya Fenerbahce, Besiktas na Sporting Lisbon, huku Leicester wakiwa tayari kukubali ofa za karibu pauni milion 18 kwa raia huo wa Algeria mwenye miaka 30. (Sky Sports)

Ajenti wa Axel Witsel anasema kiungo huyo wa kati mwenye miaka 29 raia wa Ubelgiji alikuwa akimezewa mate na Manchester United na Napoli kabla ya kujiunga na Borussia Dortmund kutokaTianjin Quanjian. (Het Laatste Nieuws, kupitia Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Albert Adomah

Aston Villa hawawezi kuzumgumzia mkataba mpya na wing'a raia wa Ghana Albert Adomah, na klabu za zamani ya mchezaji huyo mwenye miaka 30 ya Middlesbrough, na Leeds wamejulishwa kuwa sasa anapatikana. (Birmingham Mail)

Aston Villa wanakaribia kumsaini beki wa Bristol City Joe Bryan, lakini Fulham wametangaza ofa kwa mchezaji huo raia wa Uingereza mwenye miaka 24. (Bristol Post)

QPR wataanza mikakati yao ya kumsania mshambuliaji wa Brighton raia wa Israel Tomer Hemed, 31. (Argus)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Klabu ya Ujerumani Schalke wako katika mazungumzo kumsaini beki mwenye miaka 28 raia wa England Danny Rose kwa mkopo. (Sky Sports)

Chelsea wamempa kiungo wa kati mwenye miaka 23 raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko ruhusa ya kuzungumzia kuhama kwa kwenda AC Milan kwa mkopo. (Sun)

Atletico Madrid wana mpango wa kuongeza kiasia cha pesa cha kumfungua kutoka mkataba kipa wao mwenye miaka 25 Jan Oblak hadi pauni millioni 225. (AS)

Bora kutoka Jumatano

Kiungo wa kati wa Machester United raia wa Ufaransa Paul Pogba amewaaambia wachezaji wenzake kuwa anataka kuhama Old Trafford na kujiunga na Barcelona.

United wamekosa kumsaini mlinzi wa Bayern Munich Jerome Boateng. Mlinzi huyo Mjerumani alimpigia simu meneja wa United Jose Mourinho kumuambia kuwa ameshukuru kwa nia hiyo lakini hawezi akaelekea Machester. (Bild)

Haki miliki ya picha Rex Features

Tottenham walitoa ofa ya pauni milioni 25 kwa mchezaji za zamani raia wa England kikosi cha chini ya miaka 21 Jack Grealish, 22, siku ya Jumanne na wanasubiri jibu kutoka kwa Aston Villa. (Telegraph)

Everton wana uhakika wa kumsaini mlinzi wa Chelsea Mfaransa Kurt Zouma, 23, kwa mkopo. (Mirror)

Kipa wa England Jack Butland atalazimika kubaki Stoke City kwa sababu kumsainiaatakayechukua mahala pake itakuwa vigumu kwa kuwa tarehe ya mwisho inakaribia, kwa mujibu wa meneja wa Potters Gary Rowett. (Sentinel)

Crystal Palace na Fulham wote wanamtaka mshambuliaji wa Swansea City na Ghana Jordan Ayew. Mchezaji huyo wa miaka 29 anatakataa kufanya mazoezi na timu yake.(Mirror)

Mada zinazohusiana