Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 10.08.2018: Mourinho, Pogba, Kurt Zouma, Yanick Bolasies, Marcos Rojo, Raphael Varane

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images

Bodi ya Manchester United ilimwambia Jose Mourinho kwamba anafaa kukoma kuitisha pesa za kuwanunua wachezaji wapya na badala yake aangazie kuwatumia wachezaji wenye vipaji alio nao na pia kukuza wachezaji wa akademi. (Mirror)

Meneja wa United Mourinho anaamini wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amekuwa akiidhuru klabu hiyo kwa kujaribu kumuuza Mfaransa huyo mwenye miaka 25 kwa Barcelona na Juventus. (Times)

United waliikataa fursa ya kumchukua beki wa kati wa Leicester na England Harry Maguire, 25, kwa £15m mwaka jana. Lakini mwaka huu wamekuwa wakimtafuta sana na hawakufanikiwa kumnunua (Telegraph)

Haki miliki ya picha Rex Features

Kama sehemu ya maafikiano yaliyofanikisha beki wa Colombia mwenye miaka 23 Yerry Mina kuhama kutoka Barcelona hadi Everton, klabu hiyo ya Uhispania ina kifungu cha kuiwezesha kumnunua tena kwa euro 60m (£53.9m). (Marca)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Maguire

Everton watalazimika kusubiri hadi Ijumaa asubuhi kubaini iwapo ombi lao la kumtaka beki wa Ufaransa mwenye miaka 23 Kurt Zouma kutoka Chelsea kwa mkopo limekubaliwa. (Liverpool Echo)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hana shida na uamuzi wa kiungo wa kati wa Ujerumani mwenye miaka 24 Emre Can kukataa mkataba mpya na badala yake kuondoka bila ada yoyote kwenda Juventus. (Liverpool Echo)

Beki wa kushoto wa Tottenham mwenye miaka Danny Rose bado anataka sana kuhamia Paris St-Germain kwa mkopo. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Rose

Kwingineko, meneja wa Spurs Mauricio Pochettino amelaumu Brexit (uamuzi wa Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya) pamoja na ujenzi wa uwanja mpya wa klabu hiyo kama mambo yaliyochangia klabu hiyo kutofanikiwa kumnunua mchezaji yeyote dirisha la uhamisho la ulai/Agosti. (Sky Sports)

Baada ya makubaliano ya uhamisho wa mshambuliaji wa Italia anayechezea Juventus Stefano Sturaro kwenda Watford kutibuka, Sporting Lisbon wanatarajiwa sasa kumnunua mchezaji huyo mwenye miaka 25. (A Bola)

Kipa Mbelgiji mwenye miaka 26 Thibaut Courtois ambaye alihamia Real Madrid kutoka Chelsea aliufuta ujumbe wake wa kuwaafa mashabiki wa Chelsea baada yake kushutumiwa vikali na mashabiki hao na kutukanwa. (Daily Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jack Grealish

Kiungo wa kati wa Aston Villa mwenye miaka Jack Grealish anatarajiwa kutia saini mkataba ambao utakuwa na kifungu cha kumruhusu aihame klabu hiyo iwapo watashindwa kupanda daraja msimu huu. (Daily Star)

Meneja wa Burnley Sean Dyche amesema dirisha la sasa la uhamisho limekuwa mbaya zaidi kwake kushuhudi. (Lancashire Telegraph)

Mkataba wa kumpeleka beki wa Manchester United kutoka Argentina Marcos Rojo, 29, kwenda Everton ulitibuka baada ya klabu hiyo ya Old Trafford kushindwa kumnunua mchezaji wa kujaza nafasi yake. (Daily Mail)

Mchile anayechezea Manchester United Alexis Sanchez, 29, anasema alitaka klabu hiyo iwasajili wachezaji zaidi stadi kipindi cha kuhama wachezaji. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kurt Zouma

United walikuwa tayari kuvunja rekodi ya dunia na kulipa £100m kumpata beki wa Real Madrid na Ufaransa Raphael Varane, 25, hivyo ndivyo matamanio ya kumsajili mkabaji wa kati sokoni kipindi cha sasa yalivyokuwa makubwa. (Sun)

Ombi la Middlesbrough kutaka £6m kumchukua kiungo wa kati wa Everton Muhamed Besic, 25, likosa kufaulu kutokana na ada za wakala. Lakini klabu hiyo inaweza kumpata mchezaji wa Bosnia kwa mkopo. Boro pia wanatumai wataweza kumpata winga wa asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Yannick Bolasie, 29, kwa mkopo kutoka kwa Everton. (Northern Echo)

Boro pia waliwasilisha ofa zilizokataliwa za kuwataka viungo wa kati wa klabu ya Millwall Jed Wallace, 24, na George Saville, 25, siku ya mwisho ya kipindi cha kuhama wachezaji. (Sky Sports)

Bora kutoka Alhamisi

Manchester United walimkosa mlinzi wa Bayern Muninch raia wa Ujerumani mwenye miaka 29 Jerome Boateng kwa sababu walikuwa wanamtaka kwa mkopo tu. (Sun)

Boateng amekubali kujiunga na klabu ya Ufaransa ya Paris St-Germain, huku Bayern wakijiandaa kumuuza kwa pauni milioni 40.5. (Le Parisien)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jerome Boateng

Mshambuliaji wa Leicester Islam Slimani anavutia vilabu vya Fenerbahce, Besiktas na Sporting Lisbon, huku Leicester wakiwa tayari kukubali ofa za karibu pauni milion 18 kwa raia huo wa Algeria mwenye miaka 30. (Sky Sports)

Ajenti wa Axel Witsel anasema kiungo huyo wa kati mwenye miaka 29 raia wa Ubelgiji alikuwa akimezewa mate na Manchester United na Napoli kabla ya kujiunga na Borussia Dortmund kutokaTianjin Quanjian. (Het Laatste Nieuws, kupitia Goal)

Klabu ya Ujerumani Schalke wako katika mazungumzo kumsaini beki mwenye miaka 28 raia wa England Danny Rose kwa mkopo. (Sky Sports)

Chelsea wamempa kiungo wa kati mwenye miaka 23 raia wa Ufaransa Tiemoue Bakayoko ruhusa ya kuzungumzia kuhama kwa kwenda AC Milan kwa mkopo. (Sun)

Atletico Madrid wana mpango wa kuongeza kiasia cha pesa cha kumfungua kutoka mkataba kipa wao mwenye miaka 25 Jan Oblak hadi pauni millioni 225. (AS)

Mada zinazohusiana