Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 11.08.2018: Modric, Hazard, Malcom, Pogba, Dyche, Vlasic, Grealish

Luka Modric Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Luka Modric

Luka Modric ameamua kubaki Real Madrid. Kiungo huyo wa kati raia wa Croatia mwenye miaka 29 amehusishwa na kuhama kwenda Inter Milan. (AS - in Spanish)

Modric atasaini mkataba mpya na kupandisha mshara wake kufikia ule wa nahodha Sergio Ramos. (Marca)

Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba anataka kubaki kwenye klabu (RMC Sport - in French)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Kiungo wa kati wa Chelsea Tiemoue Bakayoko, 23, amekasirishwa kutokana na yeye kutokuwepo kwenye mipango ya meneja Maurizo Sarri na anatarajiwa kutolewa kwa mkopo kwa klabu ya Italia AC Milan.

Wolves wamijiwekea lengo la kishinda Ligi ya Premio katika kipindi cha miaka saba. (Times - subscription required)

Beki mpya wa Fulham mwenye miaka 24 Joe Bryan alibadili mawazo yake kuhusu kuelekea Aston Villa akiwa safarini na kikosi hicho wakati wa mazoezi baada ya kupita uchunguzi wa kiafya. (Bristol Post)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joe Bryan

Ajenti wa kiungo cha kati wa Barcelona Malcom anasema mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa Brazil alikataa kuelekea Roma kalipiza kisasi kutokana na jinsi walimtemda na mteja wake. (TuttoMercatoWeb- in Italian)

Kiungo wa kati wa Aston Villa mwenye miaka 22 Jack Grealish atapewa mkataba mpya na pauni milioni 30 za kununua mkataba wake. (Sun)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester City Stephen Ireland, 31, anafikiria kuhama Ujerumani baada ya kundoka Stoke City mwisho wa msimu. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Stephen Ireland

Bordeaux, Rennes, Saint-Etienne na Girona wote wanammezea mate wing'a wa Manchester City mwenye miaka 21 raia wa England Patrick Roberts kwa mkopo. (Sun)

Kiungo wa kati wa Croatia mwenye miaka 20 Nikola Vlasic anaratajiwa kujiunga na CSKA Moscow kwa mkopo (Sport24 - in Russian)

Meneja ya Everton Marco Silva amemuambia mshambuliaji Ademola Lookman, 20, abaki klabuni na apiganie nafasi yake. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ademola Lookman

Manchester United wamekoselewa kwa kushindwa kulipa wanafanyakazi wake wote marupurupu, licha ya kuahidi kufanya hivyo. (Telegraph)

Paris St-Germain walikataa ofa ya Manchester United kwa mshambuliaji wake raia wa Ufaransa Kylian Mbappe, 19. (Mirror)

PSG wanataka kumsaini wing'a wa Barcelona Ousmane Dembele na kumuunganisha na meneja homas Tuchel aliyemsiamia mchezaji huyo wa miaka 21 huko Borussia Dortmund. (Mail)

Bora zaidi kutoka Ijumaa

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Bodi ya Manchester United ilimwambia Jose Mourinho kwamba anafaa kukoma kuitisha pesa za kuwanunua wachezaji wapya na badala yake aangazie kuwatumia wachezaji wenye vipaji alio nao na pia kukuza wachezaji wa akademi. (Mirror)

Meneja wa United Mourinho anaamini wakala wa Paul Pogba Mino Raiola amekuwa akiidhuru klabu hiyo kwa kujaribu kumuuza Mfaransa huyo mwenye miaka 25 kwa Barcelona na Juventus. (Times)

United waliikataa fursa ya kumchukua beki wa kati wa Leicester na England Harry Maguire, 25, kwa £15m mwaka jana. Lakini mwaka huu wamekuwa wakimtafuta sana na hawakufanikiwa kumnunua (Telegraph)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Paul Pogba

Kama sehemu ya maafikiano yaliyofanikisha beki wa Colombia mwenye miaka 23 Yerry Mina kuhama kutoka Barcelona hadi Everton, klabu hiyo ya Uhispania ina kifungu cha kuiwezesha kumnunua tena kwa euro 60m (£53.9m). (Marca)

Everton watalazimika kusubiri hadi Ijumaa asubuhi kubaini iwapo ombi lao la kumtaka beki wa Ufaransa mwenye miaka 23 Kurt Zouma kutoka Chelsea kwa mkopo limekubaliwa. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Emre Can

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hana shida na uamuzi wa kiungo wa kati wa Ujerumani mwenye miaka 24 Emre Can kukataa mkataba mpya na badala yake kuondoka bila ada yoyote kwenda Juventus. (Liverpool Echo)

Beki wa kushoto wa Tottenham mwenye miaka Danny Rose bado anataka sana kuhamia Paris St-Germain kwa mkopo. (Sun)

Mada zinazohusiana