Tetesi za Soka Ulaya Jumamosi 18.08.2018: Neymar, Marchisio, Grealish, Rondon, Janssen

Neymar

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Neymar

Real Madrid waki tayari kulipa pauni milioni 270 kwa mshambualiaji wa Brazil Neymar ikiwa vikwazo vya Uefa vitawalazimisha Paris St-Germain kumuuza mchezaji huyo mwenye miaka 26. (Sport)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amekana kumwinda kiungo wa kati raia wa Italia Claudio Marchisio baada ya mchezaji huo mwenye moaka 32 koondoka Juventus. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jack Grealish

Meneja wa Aston Villa Steve Bruce anasema Tottenham wangemsaini kiungo wa kati Muingereza Jack Grealish msimu huu ikiwa wangemueendea Mapema. (Talksport)

Mshambalizi anayeichezea Newcastle kwa mkopo raia wa venezuela mwenye miaka 28 Salomon Rondon, 28, anataka kuondoka kabisa huko West Brom. (Chronicle)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alex McCarthy

Meneja wa England Gareth Southgate atamtazama kipa wa Southampton Alex McCarthy, 28, dhidi ya Everton siku ya Jumapili wakati yuko mbioni kumtafuta kipa. (Telegraph)

Matumaini ya Tottenham ya kusaini mshambuliaji raia wa Uholanzi Vincent Janssen, 24, yamezimwa baada ya kusemekana kuwa mchezaji huyo haondoki. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Demarai Gray

Wing'a wa Leicester Demarai Gray, 22, ameweka malengo yake ya kujiunga na kikosi cha England akisema kuwa hataki kuwatazama kutoka kwenye baa, (Sky Sports)

Meneja mpya wa West Ham Manuel Pellegrini anasema hakuna sababu kuhusu ni kwa nini wachezaji wake wanaweza kuogopa kuchezea uwanja wa London. (Guardian)

Meneja wa Everton Marcos Silva amefichua kuwa anataka wachezaji wake wote wazungumze Kiingereza kila wakati. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Ademola Lookman

Pia alimshauri wing'a mwenye miaka 20 Ademola Lookman kupigania nafasi yake klabuni, Baada ya raia huyo wa England kuachwa nje ya kikosi wikendi iliyopita. (Express)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp ametoa onyo kwq mchezaji yeyote ambaye atalalamika kuhusu kuachwa nje ya kikosi. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Stephy Mavididi

Mshambuliaji wa Arsenal mwenye miaka 20 raia wa England Stephy Mavididi amejiunga na Juventus baada ya kutoichezea Gunners kwenye mechi muhimu. (Sky Sports)

Wing'a wa Swansea Nathan Dyer anatafutwa na Reading ambao watanaka kumleta mchezaji huyo mwenye miaka 30 huko Madejski kwa mkopo. (Sun)

Meneja mpya wa Leeds Marcelo Bielsa anasema amekuwa kwennye mazungumzo na makocha wengine Pep Guardiola na Mauricio Pochettino kuhusu kumchukua kwa mkopo mmoja wa wachezaji wao kutoka Manchester City na Tottenham. (Yorkshire Evening Post)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pep Guardiola

Blackbun wametoa ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 8 kwa mshambuliaji wa Nottingham Forest Ben Brereton baada ya ofa yao kwa awali wa pauni milioni 6 kwa mchezaji huyo wa miaka 19 kukataliwa. (Sun)

Celtic wametoa ofa ya zaidi ya pauni milioni 13 kutoka Porto kwa kiungo wa kati Mfaransa mwenye miaka 22 Olivier Ntcham. (Goal)