Tetesi za soka Ulaya 23.08.2018 Salah, Kane, Rose, Navas, Foden, Origi, Mourinho

Mo Salah

Chanzo cha picha, Reuters

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Liverpool Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26, na mshambulaiji wa Tottenham na England Harry Kane, wa miaka 25, wote walikataa nafasi ya kujiunga na Real Madrid baada ya timu hiyo kuu ya Uhispania kumuuza Mchezaji raia wa Ureno Cristiano Ronaldo, kwa timu ya Juventus. (El Pais - in Spanish)

Mashabiki wa Manchester United wamelipia bango lililo na ujumbe wa kutaka naibu mwenyekiti mtendaji Ed Woodward aondoke na litakalo peperushwa uwanjani wakati wa mechi dhidi ya Burnley Septemba 2. (Mail)

Mlinzi wa Tottenham na England Danny Rose wanaweza kuhamishwa kwenda timu katika Ligue 1 Paris St-Germain. Mchezaji huyo mwenye miaka 28 alikataa uhamisho wa mkopo kwenda katika ligi ya Ujerumani Bundesliga timu ya Schalke msimu huu wa joto. (Evening Standard)

Lakini Tottenham bado haijapokea ombi lolote la Rose, wala la mlinzi wa Ublegiji Toby Alderweireld, mwenye umri wa miaka 29. (Talksport)

Tottenham itashauriana na mashabiki kuhusu eneo la kuchezea mechi yake ya awamu ya tatu ya kuwania taji la Carabao baada ya kuthibitishwa wiki hii kwamba hawatoweza kuutumia uwanja wa Wembley. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Keylor Navas

Manchester City inatafakari uhamisho wa dharura wa mkopo wa kipa wa Real Madrid Keylor Navas, mwenye umri wa miaka 31, baada ya Claudio Bravo, mwenye umri wa miaka 35 kujeruhiwa. (AS - in Spanish)

Mchezaji wa kiungo cha kati Phil Foden, mwenye umri wa miaka 18, huenda anatarajiwa kuitwa England huku Meneja Gareth Southgate akiripotiwa kuzungumza na Meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuhusu anavyoendelea (Sun)

Liverpool na Borussia Dortmund zinafanya mazungumzo kuhusu mkataba wa kumsajili mchezaji wa kiungo cha mbele wa Ubelgiji Divock Origi, mwenye umri wa miaka 23. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Ruben Loftus-Cheek,

Chelsea inahitaji kumshawishi mchezaji wa kiungo cha kati wa England Ruben Loftus-Cheek, kuwa ana umuhimu mkubwa kwao ili aweze kuendelea kusalia Stamford Bridge. (Mirror)

Winga wa Chelsea Lucas Piazon huenda anaelekea katika timu mpya kwenye Ligue 1 Reims kwa mkopo. Mchezaji huyo alishiriki mechi tatu kwa timu ya the Blues tangu kujiunga nayo mnamo 2011 na kuwa kuichezea Fulham kwa mkopo kwa misimu miwili iliyopita. (Sun)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Arsenal na timu ya taifa ya Ufaransa Thierry Henry, atakutana na wamiliki wa timu ya Bordeaux leo Alhamisi khusu kuwa meneja mpya. (Mirror)

Chanzo cha picha, Reuters

Mchezaji wa kiungo cha meble wa Juventus na timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo, amefichua kwamba Sir Alex Ferguson alimwambia apunguze chenga alizopiga akiwa Manchester United. (DAZN, via Manchester Evening News)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, West Ham na timu ya taifa ya England Carlton Cole, mwenye umri wa miaka 34, ametangazwa kufilisika. (Sun)

Aliyekuwa refa katika ligi ya England Bobby Madley anatarajiwa kuhamia kwenda Norway baada ya kujiuzulu wadhifa wake. (Mail)