Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 25.08.2018: Real Madrid, Liverpool, Barcelona, Hazard, Dembele, Karius

Eden hazard

Babake Eden Hazard anahofia kwamba mshambuliaji huyo wa Chelsea na ubelgiji, 27, huenda asijiunge tena na mabingwa wa Uhispania Real Madrid. (Mirror)

Besiktas inaonekana kuthibitisha kuwasili kwa kipa wa Liverpool Loris karius kwa mkopo baada ya kuchapisha picha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 ,raia wa Ujerumani katika mtandao wa Twitter-na baadaye kuiondoa. (Sky Sports)

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola ameitaka ligi ya Premia kupunguza makali ya sheria za ligi hiyo kuhusu usajili wa dharura nje ya dirisha la uhamisho baada ya juhudi zake za kutafuta kipa wa kushikilia katika siku chache zilizopita. (Telegraph)

City inataka kutatua matatizo yake ya kipa kwa kumsajili raia wa Brazil Diego Cavalieri mwenye umri wa miaka 35.

Raia huyo ambaye yuko huru alihdumu katika klabu ya Liverpool na Crystal Palace. (Globo Esporte - in Portuguese)

Kipa wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris huenda akapokonywa wadhfa wa unahodha wa klabu hiyo baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 kushtakiwa kwa kuendesha gari akiwa mlevi. (Sun)

Celtic huenda ikamuuza mshambuliaji Moussa Dembele kabla ya mwisho wa mwezi na Marseille inamnyatia mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22, raia wa Ufaransa. (La Provence - via Star)

Mkufunzi wa Paris St-Germain Thomas Tuchel amekataa kuzungumzia kuhusu uhusiano wake na beki wa Tottenham Danny Rose lakini anasema kuwa mchezaji huyo wa Uingereza ameonyesha kuwa mgumu kuanza naye mazungumzo katika siku za nyuma (Evening Standard)

Mkufunzi wa Aston Villa Steve Bruce anasema kuwa klabu yake itakuwa na hamu kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa Chelsea mwenye umri wa miaka 20 raia wa Uingereza Tammy Abraham iwapo atapatikana.(Birmingham Mail)

Bruce pia ana matumaini ya kumsajili mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie, 29, lakini mchezaji huyo wa DR Congo huenda asiwasili kwa muda unaohitajika kucheza dhidi ya Reading wikendi hii.. (Birmingham Mail)

Wolverhampton Wanderers inataka kumsaini winga wa PSG Goncalo Guedes lakini mchezaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 21 ameamua kuelekea Valenecia..(L'Equipe - via HITC)

Barcelona huenda ikamuuza kiungo wa kati wa Croatia Ivan Rakitic, 30, kwa PSG. (Evening Standard)

Klabu ya Ujerumani RB Leipzig inajiandaa kuwasilisha ombi la nne la £25m kumnunua mshambuliaji wa Everton mwenye umri wa miaka 20 Ademola Lookman. (Mirror)

Chelsea imeipatia klabu ya Uturuki ya Galatasaray ruhusa kuanzisha mazungumzo na beki wa Uingereza mwenye umri wa miaka 32 Gary Cahil. (Fotomac - via Sun)

Liverpool imesitisha mazungumzo na Borussia Dortmund kuhusu uwezekano wa kumuuza mshambuliaji wa Ubelgiji Divock Origi baada ya ya klabu hiyo ya Ujerumani kukataa ombi la Liverpool la dau la £27m . (Liverpool Echo)

Rafinha amewachwa nje ya kikosi cha Barcelona kinachoelekea Valladolid huku kukiwa na uvumi kwamba huenda mchezaji huyo wa Brazil akajiunga na klabu ya Real Betis. (Sport)

Mkufunzi wa Celtic Brendan Rodgers anataka klabu hiyo kuwasajili wachezaji watatu wapya kabla ya siku ya mwisho ya siku ya uhamisho. (Express)

Tetesi za soka Ulaya 24.08.2018

Jose Mourinho amewaambia rafiki zake kwamba angeweza kujiuzulu kutoka klabu nyingine yoyote kufikia sasa ila Manchester United. Kocha huyo mwenye umri wa miaka 55 anaarifiwa kutafshika kwa anachokiona kuwa ni ukosefu wa kuungwa mkono na kaimu mwenyekiti Ed Woodward. (Mirror)

Licha ya kutafshika, Mourinho anasalia kuwa na uwajibikaji mkubwa katika klabu hiyo ya Old Trafford. (Manchester Evening News)

Aliyekuwa mkuu wa Real Madrid Zinedine Zidane ana hamu kuipata nafasi kuiongoza Manchester United iwapo tu Mourinho ataondoka. (Mail)

Huenda ukavutiwa na hii pia:

Bin amu wa mmiliki wa Manchester City Sheikh Mansour ameshindwa kuinunua Liverpool kwa thamani ya £ bilioni 2b. (Mail)

Danny Rose wa Tottenham analengwa na Paris St-Germain wanaotaka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kabla ya kufungwa kwa dirisha la uhamisho Ulaya. (Mirror)

Real Madrid bado inashughulika kumsajili mchezaji atakayeichukua nafasi ya Cristiano Ronaldo na inaamini ina nafasi ya kumpata mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe, aliye na miaka 19. (Marca - kupitia Metro)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mbappe

Klabu hiyo ya Uhispania sasa inahisi 'huenda haitowezekana' kumsajili mojawapo ya washambuliaji wakuu katika ligi ya England katika dirisha hili la uhamisho na sasa wanaelekeza azma yao kwa mchezaji wa kiungo cha mbele wa Valencia Rodrigo, kando na Mbappe. (Independent)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Liverpool Iago Aspas, 31, anahitajika na Real Madrid na huenda akaondoka Celta Vigo kwa mkataba wa thamani ya £ milioni 35. (Super Deporte - kupitia HITC)

Real Betis wamewasilisha rasmi ombi la kumsajili mchezaji chipukizi wa Manchester City mwenye umri wa miaka 21 Oleksandr Zinchenko kwam kataba wa mkopo kwa msimu mzima, kwa mtazamo wa kumpa mkataba wa kudumu. (Mundo Deportivo - kupitia Manchester Evening News)

Arsène Wenger kuelekea Liberia Ijumaa kutuzwa na Rais George Weah

Arsène Wenger apewa makaribisho makubwa Liberia

Barcelona inajitayarisha kupokea ombi la thamani ya £81m kutoka Paris St-Germain kwa mchezaji wa kiungo cha kati raia wa Croatia Ivan Rakitic, mwenye umri wa miaka 30. (Sport - kupitia Daily Express)

Meneja Marco Silva anasema winga wa Everton Ademola Lookman ndio 'mustakabali wa wa klabu hiyo' katika jitihada za kuishawishi RB Leipzig kuacha kumfukuzia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20. (Independent)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marco Silva anasema winga wa Everton Ademola Lookman ndio 'mustakabali wa wa klabu hiyo'

Kocha mkuu wa Lyon Bruno Genesio anasema mchezaji wa kiungo cha kati anayeshambulia Nabil Fekir, 25, ameona vigumu kukubali kuwa uhamisho wake msimu huu wa joto kwenda Liverpool hakufanikiwa. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Southampton Harrison Reed anaonekana kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo kwa mkopo huku Blackburn ikionyesha hamu ya kumchukua mchezaji huyo wa miaka 23 raia wa England. (Daily Echo)

Kipa wa Man City Bravo nje kutokana na jeraha

Manchester United haina wachezaji wowote wanaoweza kuingia katika timu ya Jurgen Klopp Liverpool anasema aliyekuwa mshambuliaji wa Reds Dean Saunders. (Talksport)

United inaonekana kuwa tayari kuwapiku wapinzani Manchester City katika kumsajili Lukasz Bejger, mwenye umri wa miaka 16, kutoka Lech Poznan. (Manchester Evening News)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Georginio Wijnaldum amefichua namna meneja Jurgen Klopp alivyomtaka kujiimarisha kwa 'kujihusisha zaidi' na kuonyesha ukakamavu msimu huu. (Liverpool FC)

Mada zinazohusiana