Mchezaji wa Brazil Somalia ajiunga na al-Shabab nchini Saudia

Kiungo wa kati wa Brazil Somália anajiunga na klabu ya Saudia Al-Shabab Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa kati wa Brazil Somália anajiunga na klabu ya Saudia Al-Shabab

Somália amejiunga na al-shababa lakini sivyo unavyodhania.

Wergiton do Rosario Calmon, kwa jina maarufu Somalia ameichezea klabu ya Ufaransa ya Toulouse kwa takriban miaka mitatu, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 kutoka Brazil sasa amehamia katika klabu ya Al-Shabab nchini Saudia.

Huku ikiwa jina al-Shabab linalomaanisha Vijana kwa kiarabu sio jina baya , mitandao ya kijamii ilikuwa na haraka kulishirikisha jina hilo na kundi la kijihad mashariki mwa Afrika.

Kundi hilo linalohusishwa na lile la al-Qaeda limekuwa likipigana na serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa mataifa kwa ,muonhgo mmja uliopita na limetekeleza msururu wa mashambulizi katika eneo hilo.

Toulouse FC ilitangaza uhamisho huo na kumshukuru Somaliua kwa taaluma yake.

Kwa wengine ulinganifu huo haukuwafurahisha

Mchezaji huyo wa Brazil anaelekea Riyadh kwa kandarasi ya miaka miwili.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii