Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 28.08.2018: Pogba, Cahill, Henry, Strootman, Ramires, Grealish

Paul Pogba

Chanzo cha picha, Rex Features

Beki wa Uhispania na Barcelona Gerard Pique, 31, anasema itakuwa vyema sana iwapo kiungo wa kati wa Manchester United aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa na Ufaransa Paul Pogba, 25, atahamia Nou Camp siku zijazo. (AS)

Beki wa England anayechezea Chelsea Gary Cahill, 32, yuko tayari kusalia na kupigania nafasi yake baada ya kuonekana kuwekwa pembeni katika kikosi cha Maurizio Sarri. (Telegraph)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry, 41, anatarajiwa kuikataa nafasi ya kuwa meneja wa Bordeaux kwa sababu ya wasiwasi kuhusu ukosefu wa fedha katika klabu hiyo ya Ligue 1. (Sun)

Beki wa West Ham Reece Oxford, 19, anatafutwa kwa mkopo na klabu ya Eibar inayocheza ligi kuu Uhispania, klabu ambayo iko tayari kulipa ada ya £1.8m ya uhamisho wa mkopo. (Marca)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Gary Cahill akisherehekea awali

Kiungo wa kati wa Roma na Uholanzi Kevin Strootman, 28, anatarajiwa kufikisha kikomo kipindi cha miaka mitano ambayo amekuwa katika klabu hiyo ya Serie A na kuhamia Ufaransa kujiunga na Marseille kwa £22.6m. (Football Italia)

Kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea na Brazil Ramires, 31, anakaribia kurejea klabu yake ya zamani ya Benfica kwa mkopo kutoka klabu ya China ya Jiangsu Suning. (O Jogo)

Los Angeles Galaxy wanamtaka beki wa zamani wa Arsenal na Ivory Coast Emmanuel Eboue, 35. (Sun)

Aston Villa wanajaribu kumshawishi mshambuliaji wa England Jack Grealish, 22, atie saini mkataba wa kudumu katika klabu hiyo inayocheza ligi ya Championship baada yao kukataa kumuuza Agosti. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jack Grealish

Mshambuliaji wa Nottingham Forest Ben Brereton, 19, anajaribu kujiunga na wapinzani wao Championship Blackburn Rovers awali kwa mkopo ambao unaweza kubadilishwa kuwa mkataba wa kudumu, ada ya uhamisho wake ikiwa £7m. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Stoke City Giannelli Imbula, aliyezaliwa Ubelgiji lakini amechezea timu ya taifa ya vijana wasiozidi miaka 21 ya Ufaransa, anatakikana kwa mkopo na Rayo Vallecano, wanaocheza La Liga, Ufaransa. Stoke walivunja rekodi yao ya ununuzi wa wachezaji kumnunua mchezaji huyo mwenye miaka 25 kutoka Porto kwa £18.3m mwezi Februari 2016. (Cadena Ser)

Bora kutoka Jumatatu

Beki wa Brazil David Luiz, 31, anasema huenda angelazimika kuihama Chelsea iwapo Antonio Conte angesalia kama meneja wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mlindalango wa Liverpool Simon Mignolet, 30, anasema inashangaza kwamba klabu hiyo ya Anfield ilimruhusu kipaLoris Karius kujiunga na Besiktas ya Uturuki kwa mkopo. Mbelgiji huyo anasema hajui mustakabali wake katika klabu hiyo ya England. (Liverpool Echo)

Beki wa Tottenham Danny Rose, 28, huenda akahamia Marseille - kwa mkopo au kwa mkataba wa kudumu - katika juhudi zake za kutaka kujiimarishia nafasi ya kucheza katika timu ya taifa ya England. (Star)

Mshambuliaji wa Juventus Mario Mandzukic, 32, alikataa ofa ya kujiunga na Manchester United. (Calciomercato kupitia Sun)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mario Mandžukić alikataa kujiunga na Man Utd

Winga wa Everton Theo Walcott, ambaye hajachezeshwa timu ya taifa ya England kwa miaka miwili anasema bado hajapoteza matumani kwamba anaweza kuchezeshwa. (Independent)

West Ham wamepokea ofa kutoka kwa klabu ya Uholanzi AZ Alkmaar na klabu ya Uhispania Eibar wote wakimtaka beki wa England mwenye miaka 19 Reece Oxford. (Mail)

Tottenham walikuwa wanamtaka mshambuliaji Anthony Martial, 22, na pia kiungo wa kati Juan Mata, 30, kutoka kwa Manchester United, lakini maombi yao yakakataliwa. (Manchester Evening News)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso amesema kiungo wa kati Mfaransa Tiemoue Bakayoko - aliye nao kwa mkopo kutoka Chelsea - ni lazima ajifunze "mambo kadha ya msingi" baada ya klabu hiyo kushindwa 3-2 Napoli. (Eurosport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tiemoue Bakayoko