Diamond League: Mkenya Kipruto ashinda mbio za mita 3000 baada ya kupoteza kiatu

Kenya"s Conseslus Kipruto (L) na Soufiane El Bakkali wa Morocco katika mbio za mita 3000 kufruka viunzi na maji katika mbio za IAAF Diamond League Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kipruto anasema kuwa alipata motisha zaidi baada ya kupoteza kiatu ili kushinda mbio hizo

Mwanariadha wa Kenyan Conseslus Kipruto alikaidi pigo la kupoiteza kiatu mapema ili kuibuka mshindi wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika ligi ya almasi ya IAAF Diamond League mjini Zurich, nchini Switzerland.

Baada ya kupiga kona moja ya uwanja kiatu chake cha kushoto kilitoka lakini hilo halikumzuia .

'' Ilikuwa kisirani .Lakini nilipata motisha ya kupigana zaidi ili niendelee vyema'', alisema baadaye.

Kipruto ndio bingwa wa Olimpiki na na wadunia katika mbio za kuruka viunzi na maji. Alimpita Soufiane El Bakkali katika mita za mwisho baada ya kuruka kiunzi cha mwisho akiwa wa pili.

''Nimepata jeraha kwa sababu nilipoteza kiatu changu, alisema baada ya kukamilisha mbio hizo''.

Baadaye alituma ujumbe wa twitter:

Ilikuwa vigumu na uchungu kukimbia bila viatu, lakini nilikuwa na moyo wa ujasiri ya kutokubali kushindwa , mashabiki walikuwa wazuri na nikaamua kuendelea ili kushinda.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kipruto aruka kiunzi cha mwisho na Soufiane El Bakkali wa Morocco.

Baada ya mbio hizo mwanariadha huyo wa Kenya aliguchia na kuondoka katika uwanja akiwapungia mkono mashabiki.

Wakenya katika mitandao ya kijamii ikiwemo naibu rais William Ruto wamekuwa wakimpongeza Kipruto kwa ushindi huo

Mada zinazohusiana