Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 01.09.2018: Arsenal, Man United, Chelsea, Tottenham, Ozil, Anthorny Martial, Jurgen Klopp, Unai Emery

Mesut Ozil

Chanzo cha picha, Getty Images

Mkufunzi wa Arsenal Unai Emery amekana kwamba amekosana na kiungo wa kati wa Ujerumani Mesut Ozil, lakini anasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 anahitaji kucheza maeneo tofauti katika klabu hiyo.. (Guardian)

Manchester United haijakiubaliana kuhusu mkataba mpya wa kumzuia mshambuliaji wake Anthony Martial ,22, kuondoka katika uwanja wa Old Trafford , huku raia huyo wa Ufaransa akiendelea na mazungumzo na klabu hiyo.(Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

West Brom ilifeli kumnunua kiungo wa kati wa Blackburn Rovers na Uingereza Bradley Dack, 24 kwa dau lililovunja rekodi la £15m. (Sun)

Everton imekataa dau la muda wa mwisho la £25m kutoka RB Leipzig kumnunua mshambuliaji Ademola Lookman, 20, huku klabu hiyo ya Bundesliga ikitaka kumnunua raia huyo wa Uingereza kurudi katika uwanja wa Red Bull Arena. (90min)

Jurgen Klopp amemuonya kipa wa Liverpool Simon Mignolet, 30, kuwa tayari kuchezeshwa baada ya kipa mpya Alisson. Raia huyo wa Ubelgiji sasa atachezeshwa baada ya kipa Alisson. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mmiliki wa Watford Gino Pozzo amekataa dau la £125m kuuza asilimia 35 ya klabu hiyo kwa Prolific Media Holdings, ambayo imekita kambi mjini New York. (Times - subscription required)

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa hatojaribu kuwashawishi watu kusalia ambao hawataki kusalia akiongezea kwamba sio tatizo iwapo klabu hiyo itapoteza wachezaji wawili au watatu kwa kuwa klabu hiyo ina wachezaji chungu nzima katika taasisi yao ya mafunzo ya soka.(Telegraph)

Pochettino amewataka mashabiki kuwa na subra huku tarehe na uwanja wa mechi ya Carabao dhidi ya Watford ikipangwa (Mail)

Spurs na Manchester City wamekubaliana kubadilisha tarehe ya mechi yao kutoka Jumapili 28 Oktoba hadi Jumatatu 27 lakini wanahitaji ligi ya Premia kuidhinisha uamuzi huo. (Times - subscription required)

Chanzo cha picha, Getty Images

Afisa mpya mtendaji wa klabu ya Aston Villa Christian Purslow anatarajiwa kuanza mazungumzo na kiungo wa kati Jack Grealish kuhusu mkataba mpya wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Wolves Raul Jimenez, 27, amekana madai kwamba makubaliano yake ya kuhamia West ham yalivunjika baada ya kulala sana. (Express)

Beki wa Portugal Diogo Dalot, 19, ameichezea mara ya kwanza Man United tangu uhamisho wake wa dau la £19m akiichezea timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 kwa dakika 79 (Manchester United website)

John Terry na Jack Grealish walisaidia kumshawishi mshambuliaji wa Uingereza na Chelsea Tammy Abraham, 20, kujiunga na Aston Villa kwa mkopo. (Express and Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakati huohuo kiungo wa kati wa Armenian Henrikh Mkhitaryan, 29, huenda asiichezee Arsenal wakati watakapocheza dhidi ya Qarabag FK katika kombe la Yuropa kwa sababu ya mgogoro wa kisiasa kati ya Armenia na Azerbaijan. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Jurgen Klopp hajakubali kwamba winga wa Liverpool Mohamed Salah, 26, bado anataka kuichezea timu yake ya taifa na kwamba anatumai kwamba suluhu mwafaka itaangaziwa kuhusu mgogoro wake na shirikisho la soka nchini Misri.(Mail)

Maurizio Sarri anasema kuwa kiungo wakati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 22, anahitaji kuimarika kiufundi ili kuweza kushiriki katika kikosi cha kwanza cha timu. (Metro)