Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 03.09.2018: Pellegrini, de Dea, Mourinho, Ronaldo, Becker

Manuel Pellegrini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manuel Pellegrini akalia kuti kavu West Ham.

Kocha wa West Ham Manuel Pellegrini hayupo kwenye hatari ya kufurushwa na waajiri wake licha ya kupokea vichapo vine mfululizo. (Mirror)

Kipa raia wa Uhispania David de Gea, 27, anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu yake ya Manchester United ambapo atapokea mshahara wa £350,000 kwa wiki. (Sun)

Mshambuliaji wa klabu ya Paris St-Germain na timu ya Taifa ya Brazil Neymar, 26, adaiwa kupendelea kujiunga na Chelsea ama Arsenal lakini si timu mbili hasimu za jiji la Manchester. (Express)

Kiungo wa klabu ya Tottenham na nchi ya Ubelgiji Mousa Dembele, 31, anatarajiwa kwenda kusakata kabumbu Uchina mwezi Januari kwenye dirisha dogo la usajili. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Kocha wa Manchester United Jose Mourinho amesema suala la Cristiano Ronaldo kurudi Old Traford wala hailkuwepo kwenye meza ya mazungumzo. Rodaldo amejiunga na Juventus akitokea Real Madrid. (Sky Sports)

Cristiano Ronaldo bado hajaifungia goli Juventus lakini mtoto wakw mwenye miaka nane mwisho wa juma liliopita amepachika magoli manne kwenye moja ya timu za watoto za klabu hiyo. (Marca)

Mlinzi wa klabu ya Arsenal na Ujerumani Shkodran Mustafi anaweza akaadhibiwa na Chama cha Mpira (FA) kwa namna alivyoshangilia goli lake dhidi ya Cardiff siku ya Jumapili. (Mirror)

Uhusiano wa kocha wa Manchester City Pep na winga Leroy Sane, 22, kumewaogofya wachezaji wengine wa timu hiyo, hususan katika kupata nafasi ya kucheza. (London Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uzembe wa Becker uliipatia Leicester goli la kufutia machozi.

Beki wa Liverpool Joe Gomez amempigia chapuo kipa Alisson Becker licha ya kosa alilolifanya kwenye mechi dhidi ya Leicester. (Goal)

Kocha wa zamani timu ya taifa ya England amesema kuwa "alichanganyikiwa" baada ya kufutwa kazi ya kuinoa timu ya taifa lake. (Talksport)

Mshambuliaji wa Danny Ings ameweka dau na mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah kuwa yeye Ings atafunga magoli mengi kuliko Salah msimu huu. (London Evening Standard)