Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 04.09.2018: Mourinho, Pogba, Terry, Modric, Alisson, Kompany, Ronaldo, Messi

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ametania kuwa hana hofu kuwa atapoteza kazi yake kwa sababu inaweza kaigharimu klabu pesa nyinyi kumfuta. (La Repubblica via Daily Telegraph)

Meneja wa Aston Villa Steve Bruce anataka kumsaini tena mlinzi wa zamaniawa England mwenye miaka 37 John Terry. Sun

Sporting Lisbon itampa mkataba mpya mshambulizi raia wa Cape Verde mwenye miaka 20 Jovane Cabral na kuongeza pesa na kumwezesha kukata mkataba wake hadi pauni milioni 40.5 wakati Barcelona wanammzea mate. (Ojogo - in Portuguese)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Luka Modric

Fifa wamewaandikia Inter Milan na Real Madrid kusema kwa haiwezi kuchuakua hatua kufuata malamiko ya klabuahiyo ya Uhispania kuhusu kumzungumzia kinyume na sheria kiungo wa kati ria wa Croatia. Luka Modric. (Gazzetta dello Sport)

Manchester City wako tayaria kungoja hadi msimu wa msimu kabla ya kumpa ofa mlinzi Mbelgiji mwenye miaka 32 Vincent Kompany mpya. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paul Pogba

Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba amekiambia klabu kuwa anataka kurudi Juventus mwezi Januari. (Express)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema hana mipango wa kuwabadilisha makipa wake wakti wa ligi ya mabingwa huku kipa Mbrazil mwenye miaka 25 akitarajiwa kucheza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lionel Messi

Mshambulizi wa Barcelona mwenye miaka 31 raia wa Argentina Lionel Messi anasema alishangazwa na uamuzi wa mshambuliaji mwenye miaka 33 wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kuondoka Real Madrid kwenda Juventus. (AS)

Mtoto wa Ronaldo alifunga mara nne kwenye timu ya Juventus wa wachezaji walio chini ya miaka 9. (Mirror)

Messi anasema Madrid wamebaki dhaifu baada ya kuondoka Ronaldo na wakati huu ndio Barcelona inahitaji kushinda ubingwa tena. (El Pais - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Xavi

Mchezaji mpya wa Barecelona mwenye miaka 22 Arthur, kiungo wa kati raia wa Brazil ambaye alijtoka huko Gremio anamkumbusha Messi kuhusu aliyekuwa kiungo wa kati wa Barcelona na Uhispania Xavi. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Rais wa Bayern Munich Uli Hoeness anasema Paris St-Germain inastahili kumfuta mkurugezni wa michezo Antero Henrique kutokana na njia alikuwa akimsaini mlnzi wa Bayern Jerome Boateng na kiungo wa kati mreno Renato Sanches. (Kicker - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Papy Djilobodji

Sunderland bado wanajaribu kumuuza mlinzi mwenye miaka 29 raia wa senegal Papy Djilobodji na kiungo wa kati raia wa Gabon mwenye miaka 24 Ibrahim Ndong, lakini jlabu imekataa kuwalipa kwa kuwa hakurudi kwenye mazoezi. (Sunderland Echo)

Sunderland wanatathmini kumchukulia hatua za kisheria Djilobodji kwa kukataa kurudi. (Mirror)

Wafadhili wa kamari watapigwa marufuku kutoka Wembley ikiwa uwanja huo utunzwa kwa mmiliki mpya chini ya masharti yaliyowekwa na serikali. (Times - subscription required)