Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 05.09.2018: Pogba, Alli, Pavard, Morata, Pellegrini

Pogba, Alli, Pavard, Morata, Pellegrini

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pogba, Alli, Pavard, Morata, Pellegrini

Luiz Suarez anasema Paul Pogba atakaribishwa huko Barcelona wakati mchezaji huyo wa miaka 25 wa Manchester United anazidi kuhusishwa na kuhama kutoka Old Trafford. (ESPN)

Lakini pia Pogba anataka kucheza chini ya usimamizi wake Zinedine Zidane siku za usoni, wakati ripoti zikesema kuwa United wanaweza kumwinda meneja huyo wa zamani wa Real Madrid kuchukua mahala pake Jose Mourinho. (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zinedine Zidane

Vilabu vikubwa saba vikiwemo wa ligi ya Premio, Manchester City, Chelsea, Manchester United na Liverpool-vimetumia zaidi ya dola bilioni moja kuwanunua wachezaji tangu mwaka 2010. (Daily Mail)

Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui amepuuzilia mbali kuhami klabu hiyo wachezaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, na Kylian Mbappe, 19. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Neymar

Mlinzi wa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia Benjamin Pavard, 22, anasema hajafikia makubaliano yoyote ya kujiunga na Bayern Minich kutoka Stuttgart. (Sky Sports)

Mchezaji wa miaka 25 Mhispania Alvaro Morata anasema msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake. (Marca - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Manuel Pellegrini

West Ham watamlipa Manuel Pellegrini pauni milioni 15 ikiwa watamfuta meneja huyo wao raia wa Chile. (Times - subscription required)

Nyota wa Spurs na England Dele Alli, 22, amefichua jinsi mkufu aliopewa na dereva wa teksi nchini Urusi ulichangia awe na bahati nzuri. (Standard)

Ligi ya Premio inataka serikali kufuta vuzuizi vyote vya kuwasaini wachezaji wa kigeni kufuatia hofu kuwa Brexit itaathiri umaarufu wa ligi hiyo. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jordan Henderson

Nahodha wa Liverpool Jordan Henderson anasema bado anahitaji kuimarika baada ya mchezaji huyo wa miaka 28 kusaini mkataba mpya huko Anfield. (Sky Sports)

Arsenal inahusishwa na kuhama kwa ghafla mlinzi wa zamani wa Atletico Madrid na Chelsea Filipe Luis, 33, mwezi Januari. (Mirror)

Ajenti Laurent Koscielny anasema mlinzi huyo mwenye miaka 32 raia wa Ufaransa alikuwa akitathmini kuondoka Arsenal kabla ya kupata jeraha mwezi Mei. (ESPN)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Unai Emery

Kikosi cha kina dada cha Crystal Palace kimeambiwa kuwa ni lazima kipate ufadhili wa pauni milioni 250 ikiwa kinataka kuendelea kuchezea klabu hiyo. (Guardian)

Baadhi ya maafisa wa juu kwenye klabu ya Arsenal akiwemo kocha mkuu Unai Emery, wanazidi kuwa na wasiwasi kutokana na sintofahamu ya hatma yake mkurugenzi mkuu Ivan Gazidis. (Times - subscription required)

Everton wanataraji kuwa James McCarthy atarejea mazoezini kabla ya mwisho wa Septemba wakati mchezaji huyo wa miaka 27 atarudi baada ya kupata jeraha.

Bora kutoka Jumanne

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefanya mzaha kuwa hana hofu atapoteza kazi yake kwa sababu inaweza kuigharimu klabu pesa nyinyi kumfuta. (La Repubblica via Daily Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho

Meneja wa Aston Villa Steve Bruce anataka kumsaini tena mlinzi wa zamani wa England mwenye miaka 37 John Terry. Sun

Sporting Lisbon itampa mkataba mpya mshambulizi raia wa Cape Verde mwenye miaka 20 Jovane Cabral na kuongeza pesa ya kumwezesha kupunguza mkataba wake hadi pauni milioni 40.5 wakati Barcelona wanammezea mate. (Ojogo - in Portuguese)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Luka Modric

Fifa wamewaandikia Inter Milan na Real Madrid kusema kuwa haiwezi kuchukua hatua kufuata malamishi ya klabu hiyo ya Uhispania kuhusu kumzungumzia kinyume na sheria kiungo wa kati raia wa Croatia. Luka Modric. (Gazzetta dello Sport)

Manchester City wako tayari kusubiri hadi msimu ujao kabla ya kumpa ofa mpya mlinzi Mbelgiji mwenye miaka 32 Vincent Kompany. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Vincent Kompany

Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba amekiambia klabu kuwa anataka kurudi Juventus mwezi Januari. (Express)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema hana mipango wa kuwabadilisha makipa wake wakti wa ligi ya mabingwa huku kipa Mbrazil mwenye miaka 25 akitarajiwa kucheza