Thomas Gronnemark ndiye mwenye kazi mbaya zaidi katika kandanda duniani?

Mkufunzi wa kurusha mpira uwanjani Thomas Gronnemark

Chanzo cha picha, Thomas Gronnemark

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa kurusha mpira uwanjani Thomas Gronnemark akishirikiana na klabu ya Denmark FC Midtjylland

Thomas Gronnemark aliwashangaza wengi alipowasili katika klabu ya Liverpool msimu huu baada ya msimu ulioshirikisha matumizi ya juu kuwanunua kipa Alisson, kiungo wa kati Fabinho na Keita.

Hata mkufunzi Jurgen Klopp alikiri kwamba hajawahi kusikia kuhusu mkufunzi wa kurusha mipira uwanjani kabla ya kumuajiri raia huyo wa Denmark.

Usajili wa raia huyo mwenye umri wa miaka 42 ambaye anashikilia rekodi ya urushaji mrefu wa mipira duniani akiwa amewahi kurusha mita 51.33, ulizuia hisia na kufanyiwa mzaha na mchanganuzi wa runinga Andy Gray.

"Najua ni kazi mbaya zaidi duniani ," Gronnemark, ambaye anahisi ndiye mtaalamu wa kwanza wa kurusha mipira aliambia BBC Sport.

Kiungo wa kati wa zamani wa klabu ya Stoke Rory Delap huenda ndiye mrushaji mpira bora zaidi katika ligi ya Uingereza , lakini Gronnemark anasema kuwa kazi yake ya muda mfupi katika klabu ya Liverpool sio tu kuifanya Liverpool kuwa kama Stoke City.

Kama anavyoelezea kuna zaidi ya kinachoonekana kwa urushaji huo na kuna mbinu ambazo zikitumiwa zinaweza kusababisha goli na hata kuokoa timu.

Tayari ameanza kuleta tofauti katika klabu ya Liverpool

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Liverpool ilirusha mipira 54 katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Leicester Jumamosi

"Niliona Joe Gomez akirusha vizuri mipira yake akiichezea Liverpool hali ambayo nilikuwa sijawahi kuiona awali alikuwa akiurusha mpira huo mahala anapotaka'', alisema mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright.

Inaonekana kana kwamba yeye Gronnemark amemfundisha kitu. Lazima Liverpool watafaidika na urushaji huo.

Klopp anaamini kwamba Gronnemark ameleta tofauti na kazi yake katika Melwood.

"Kwa kweli nilikuwa sijawahi kusikia kuhusu mkufunzi mrushaji mipira, alisema Mejrumani huyo. Wakati niliposikia kuhusu Thomas ilikuwa wazi kwamba nilitaka kumuona.

Nilipokutana naye ilikuwa asilimia 100 nilitaka kumuajiri. Gronnemark ambaye amekuwa akifanya kazi na timu tangu 2004, alisema kwamba Klopp aliwasiliana naye kwa sababu alitaka kujua kazi yake ni nini haswa na anasema kuwa ni ndoto kubwa.

'Iwapo ningekuwa beki nisingependelea kuwa mpinzani wa mipira inayorushwa na Gomes', alisema Gronnemark.

Kwa jumla dhidi ya Liverpool nisingependelea kutoa mpira nje ili urushwe. Sisemi kwamba Liverpool itarusha mipira mingi mirefu , lakini huwezi kujua ni saa ngapi wanaweza kufanya hivyo.

Sayansi ya kurusha mipira

Chanzo cha picha, Thomas Gronnemark

Maelezo ya picha,

Thomas Gronnemark ni mwanariadha wa zamani

Gronnemark anakadiria kwamba kuna kati ya mipira 40-50 inayorushwa katika mechi na katika mechi ya Jumamosi dhidi ya Leicester Liverpool ilirusha mipra 54, jukumu lao na muhimu wao ni kwamba , anasema inadharauliwa ikilinganishwa na mipira mingine ya nidhamu.