Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 06.09.2018: Pogba, Rabiot, Vertonghen, Maguire, Rakitic, Asensio, Hoolahan

Chanzo cha picha, Getty Images
Pep Guardiola
Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba hawezi kulazimisha kuhama kwake mwezi Januari. (Mirror)
Liverpool wamefanya mawasiliano na mama na pia ajenti kwa kiungo wa kati wa Paris St-Germain mwenye miaka 23 Adrien Rabiot. (ESPN)
Meneja wa Manchester City' Mhispania Pep Guardiola amepiga marufuku simu kwenye maeneo ya kufanyia mazoezi ya klabu hiyo. (Daily Mail)
Chanzo cha picha, Getty Images
Jan Vertonghen
Mlinzi wa Tottenham mwenye miaka 31 Jan Vertonghen anatarajia klabu kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingine mmoja. (Evening Standard)
Mlinzi wa England na Leicester Harry Maguire, 25, anasema haelewi jinsi mataifa ya Uefa hufanya kazi. (Telegraph)
Aliyekuwa kiungo wa kati wa Norwich na Jamhuri ya Ireland Wes Hoolahan, 36, anafanya mazoezi na West Brom na atijiunga kama mchezaji huru. (Eastern Daily Press)
Chanzo cha picha, Getty Images
Wes Hoolahan
Kiungo wa kati wa Barcelona raia wa Croatia mwenye miaka 30 Ivan Rakitic anasema vilabu vikubwa vilikuwa vinataka kumsaini msimu huu, lakini aliamua kubaki Uhispania. (Novi List - in Croatian)
PSV wanataka kumsaini kiungo wa kati wa Real Monarchs mmarekani Richard Ledezma 17, (Eindhovens Dagblad - in Dutch)
Klabu ya Ureno ya Benfica itapigwa marufuku ya kucheza kwa hadi miaka mitatu baada ya kulaumiwa kwa uhalifu unaohusu kuingilia mifumo ya sheria ya nchi. (Correio da Manha - in Portuguese)
Chanzo cha picha, Getty Images
Marco Asensio
Real Madrid wamempa ofa mshambuliaji Marco Asensio ya jesi namba 7 ya klabu hicho lakini mchezaji huyo wa miaka 22 amekataa. (Cope - in Spanish)
Fulham wanataka kumpa kipa raia wa England mwenye miaka 26 Marcus Buttinelli mkataba mpya. (Sun)
Bora zaidi kutoka Jumatano
Chanzo cha picha, Getty Images
Paul Pogba
Luiz Suarez anasema Paul Pogba atakaribishwa huko Barcelona wakati mchezaji huyo wa miaka 25 wa Manchester United anazidi kuhusishwa na kuhama kutoka Old Trafford. (ESPN)
Lakini pia Pogba anataka kucheza chini ya usimamizi wake Zinedine Zidane siku za usoni, wakati ripoti zikisema kuwa United wanaweza kumwinda meneja huyo wa zamani wa Real Madrid kuchukua mahala pake Jose Mourinho. (Metro)
Chanzo cha picha, Getty Images
Zinedine Zidane
Vilabu vikubwa saba vikiwemo wa ligi ya Premio, Manchester City, Chelsea, Manchester United na Liverpool vimetumia zaidi ya dola bilioni moja kuwanunua wachezaji tangu mwaka 2010. (Daily Mail)
Meneja wa Real Madrid Julen Lopetegui amepuuzilia mbali kuhami klabu hiyo, wachezaji wa Paris St-Germain Neymar, 26, na Kylian Mbappe,
Chanzo cha picha, Getty Images
Neymar
Mlinzi wa kikosi cha Ufaransa kilichoshinda Kombe la Dunia Benjamin Pavard, 22, anasema hajafikia makubaliano yoyote ya kujiunga na Bayern Minich kutoka Stuttgart. (Sky Sports)
Mchezaji wa miaka 25 Mhispania Alvaro Morata anasema msimu uliopita ulikuwa mgumu kwake. (Marca - in Spanish)