Mkusanyiko wa habari muhimu za michezo Alhamisi: Leroy Sane, Wilfried Zaha, David Becham, Shaw

Leroy Sane na kocha wa timu ya Ujerumani

Leroy Sane atalazimika kuimarisha tabia yake kwa yeye kuweza kufanikiwa kulingana na mchezaji mwenza wa Ujerumani Toni Kroos.

Sane mwenye umri wa miaka 22 aliwachwa nje ya kikosi cha Ujerumani cha kombe la dunia lakini amerudi kwa mechi ya Uefa dhidi ya Ufaransa mbali na mechi ya kirafiki ya siku ya Jumapili dhidi ya Peru.

Lakini bado hajaanzishwa katika klabu yake ya City msimu huu na aliwachwa nje siku ya Jumamosi.

Mara nyengine unapata anavyohisi kutokana na tabia yake na ni muhimu sana iwapo tunashinda au kupoteza.

''Ni mchezaji ambaye ana kila kitu unachohitaji kuwa mchezaji bora, lakini mara nyengine lazima umwambie kwamba ni sharti aonyeshe kiwango cha juu cha mchezo'', aliongeza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Real Madrid.

Sane alishinda taji la mchezaji chipukizi la 2017-18 baada ya kufunga magoli 10 na kutoa usaidizi wa mabao 15 katika ligi ya Uingereza msimu uliopita

Zaha atoa msaada kwa timu ya wanawake ya Crystal Palace

Wilfried Zaha anatarajiwa kutoa mchangu mkubwa kusaidia wanadada wa klabu ya Crystal palace.

Hatua hiyo ya winga wa Crystal Palace inafuatia ripoti kwamba kikosi cha pili cha klabu hiyo kimeambiwa kulipoa £250 kila mmoja wao la sivyo waondoke katika klabu hiyo.

Timu ya wanawake ya Crystal Palace ambayo inacheza katika ligi ya wanawake amesema kuwa ripoti hiyo ya Guardian sio ya kweli.

Klabu hiyo imesema kuwa inamshukuru Zaha mwenye umri wa miaka 25, ambaye mwezi Agosti alisaini kandarasi mpya yenye thamani ya £130,000 kwa wiki.

Jina la klabu mpya ya Becham latajwa

Klabu ya David Beckham ya ligi ya Major League Soccer team nchini Marekani sasa itapatiwa jina la Club Internacional de Futbol Miami - ama Inter Miami CF - na tayari chapa ya klabu hiyo imezinduliwa.

Inter Miami itaanza kucheza katika ligi ya MLS 2020 baada ya kupewa kandarasi ya kuendelea mnamo mwezi Januari.

Chapa hiyo ina rangi ya waridi, nyeusi na nyeupe, ikishirikisha jua lenye miale saba. Hii ni siku nzuri kwangu na timu yote, alisema Becham.

Mchezaji huyo wa zamani wa manchester United, Real Madrid, Paris St Germain pamoja na AC Milan ambaye ni mmiliki na rais aliongezea: Tunachukua hatua nyengine muhimu kuimarisha klabu yetu na leo ni siku muhimu katika historia ya klabu ya Club Internacional de Futbol Miami."

'Karibu nipoteze mguu wangu'

Chanzo cha picha, Empics

Beki wa Manchester United Luke Shaw anasema kuwa karibu apoteze mguu wake baada ya kuvunjika maeneo mawili 2015.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 , alikosa msimu wote baada ya kupata jeraha katika mechi ya ligi ya vilabu bingwa ambapo walipoteza 2-1 dhidi ya PSV Eidhoven.

Baada ya kuitwa na Uingereza katika mechi za mwezi huu dhidi ya Uhispania na Switzerland , Shaw alisema kuwa anahisi vyema kupata fursa ya kuwa katika kikosi hicho.

''Nilikuwa na matatizo chungu nzima na mguu wangu huo ndio ulionipatia wakati mgumu zaidi katika kazi yangu''.

''Hakuna mtu anayejua lakini karibu nipoteza mguu wangu, Sikujua hadi baada ya miezi sita ndiposa daktari akaniambia''