Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 07.09.2018: Usmanov, Charlton, Ceballos, Klopp, Jorginho

Alisher Usmanov

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alisher Usmanov

Aliyekuwa mshika dau kwenye klabu ya Arsenal Alisher Usmanov anataka kuelekea sasa klabu ya Charlton Athletic baada ya kuuza hisa zake huko Arsenal za thamani ya pauni milioni 600. (Mirror)

Ajenti wa kiungo wa kati raiawa Italia Jorginho amethibitisha kuwa mchezaji huyo wa miaka 26 alikubali kujiunga na Manchester City msimu huu lakini akajiunga na Chelsea kwa kuwa City walishindwa kukubaliana mkataba na Napoli. (Metro)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jorginho

Kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 22 Dani Ceballos anasema angeondoka klabuni ikiwa Zenedine Zidane angebaki kama meneja. (Marca)

Mlinzi Mskochi Russell Martin, 32 amejiunga na mchezaji mwenzake wa zamani huko Norwich, Wes Hoolahan, 36, kwa majaribio huko West Brom. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jurgen Klopp

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp huwaambia wachezaji kujifunza lugha ya Kiingereza wakati wanajiunga na klabu hiyo. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Liverpool na England Jordan Henderson, 28, anasema alitazama marudio ya nusu ya fainali katika kombe la dunia nchini Urusi ambapo walishindwa na Croatia ili kujifunza. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kieran Trippier

Beki wa Tottenham na England mwenye miaka 27 Kieran Trippier anasema ametazama bao lake wakati wa mechi hiyo kama mara 100. (Sun)

Manchester City wamewashinda Tottenham na Chelsea kumsaini kipa mwenye miaka 16 Gavin Bazunu kwa pauni 420,000 kutoka Shamrock Rovers. (Telegraph)

Kiungo wa kati wa Real Madrid mwenye miaka 25 Isco alikataa kujibu swali kwenye mkutano na waandishi habari, akimuambia ripota. "Utaandika chenye unataka, kwa nini nikujibu? hatutaki watu ambao kila mara wanatukusoa." (El Pais - in Spanish)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dani Osvaldo

Wolfsburg wamemaliza mkataba na Kaylen Hinds baada mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal mwenye miaka 20 kutoweka mapema msimu huu akidai kuwa alikuwa na matatizo na pasipoti yake. (ESPN)

Mshambuliaji wa zamani wa Southampton na Italia Dani Osvaldo anasema aliacha kandanda na kuwa muimbaji kwenye bendi kwa sababu alitaka kuwa huru. (Sun)

Kocha wa Burnely Michael Duff anatarajiwa kutajwa kuwa meneja mpya wa Cheltenham Town. (Gloucestershire Live)

Bora kutoka Alhamisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pep Guardiola

Kiungo wa kati wa Manchester United mwenye miaka 25 Paul Pogba hawezi kulazimisha kuhama kwake mwezi Januari. (Mirror)

Liverpool wamefanya mawasiliano na mama na pia ajenti kwa kiungo wa kati wa Paris St-Germain mwenye miaka 23 Adrien Rabiot. (ESPN)

Meneja wa Manchester City' Mhispania Pep Guardiola amepiga marufuku simu kwenye maeneo ya kufanyia mazoezi ya klabu hiyo. (Daily Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jan Vertonghen

Mlinzi wa Tottenham mwenye miaka 31 Jan Vertonghen anatarajia klabu kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingine mmoja. (Evening Standard)

Mlinzi wa England na Leicester Harry Maguire, 25, anasema haelewi jinsi mataifa ya Uefa hufanya kazi. (Telegraph)

Aliyekuwa kiungo wa kati wa Norwich na Jamhuri ya Ireland Wes Hoolahan, 36, anafanya mazoezi na West Brom na atijiunga kama mchezaji huru. (Eastern Daily Press)