Diego Maradona: Achaguliwa meneja wa timu ya daraja la pili Mexico

Diego Maradona

Chanzo cha picha, @Dorados on Twitter

Maelezo ya picha,

Dorados wanafahamika kwa umaarufu kama 'Samaki wakuu'

Bingwa wa soka kutoka Argentina Diego Maradona ameteuliwa kuwa meneja wa timu ya daraja la pili nchini Mexico Dorados de Sinaloa.

Mshindi huyo wa kombe la dunia mwenye umri wa miaka 57 aliwahi kucheza mara 91 kwa nchi yake kati ya 1977 na 1994 na pia ameifunza timu hiyo ya taifa tangu 2008 hadi 2010.

Mara ya mwisho kukifunza klabu ilikuwa ni Al-Fujairah katika Umoja wa falme za kiarabu mkataba uliomalizika April.

Vyombo vya habari Mexico vinadai Maradona ameajiriwa kuichukuwa nafasi ya Francisco Gamez, aliyefutwa kazi kama kocha mnamo Alhamisi.

Katika kanda fupi ya video kwenye mtandao wa kijamii, klabu hiyo iliweka ujumbe wa kumkaribisha Maradona uliosema 'Karibu Diego', na 'Timiza 10', nambari iliyokuwa kwenye jezi ya Maradona alipokuwa mchezaji.

Maradona alizichezea timu za Argentinos Juniors, Boca Juniors, Barcelona na Napoli miongoni mwa timu nyingine alipokuwa akicheza soka ya kulipwa na atazamwa na wengi kama mojawapo ya wachezaji bora wa soka.

Alilishinda taji la Kombe la dunia mnamo 1986 kwa niaba ya taifa lake, ambaye pia aliwahi kuifunza timu hiyo ya taifa kushiriki mashindano hayo ya KOmbe la Dunia mnamo 2010 nchni Afrika ksuini.

Dorados kiliundwa 2003 na mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola aliwahi kuichezea kwa miezi 6 mnamo 1996.