Paul Pogba: Kiungo wa kati wa Manchester United anasema kutakuwa na mazungumzo kuhusu hatma yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Manchester United boss Jose Mourinho broke the world transfer fee record to sign Paul Pogba in August 2016
Kiungo wa kati wa Manchester United Paul Pogba anaamini kutakuwa na mazungumzo huku kukiwa na mjadala kuhusu hatma yake Old Trafford.
Mchezaji huyo hakuwa akichezeshwa katika kikosi cha kwanza msimu uliopita hatua iliomuhusisha na klabu za Juventus, ama Barcelona msimu huu.
Siku ya Jumatano, Pogba alizua uvumi wakati aliposema kuwa: Nani anayejua kitakachofanyika katika miezi michache ijayo.
Hatahivyo, siku ya Alhamisi alisema: Sio mimi ninayezungumza. Najaribu kufanya kazi yangu na kuimarisha maumbile yangu kimchezo.
Mshindi hyo wa kombe la Dunia alikuwa akizungumza wakati wa sare ya 0-0 dhidi ya Ujerumani katika mechi yao ya ufunguzi ya Uefa National League.
Alipoulizwa iwapo alikuwa amechoshwa na uvumi uliokuwa ukisambaa , alijibu: Nilirudi kuchelewa kutoka kwa kombe la dunia, hivyobasi najaribu kucheza vizuri zaidi.
Alipoulizwa kuhusu uhusiano wake na Mourinho, Pogba alijibu: Tuna uhusiano mzuri wa mkufunzi na mchezaji , na huo ndio ukweli.
''Kitu kimoja ambacho nitawahakikishia ni kwamba nitacheza asilimia 100-licha ya mkufunzi yeyote mimi hucheza asilimia 100. Siwezi kusema zaidi''.
Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha vijana katika timu ya Man United alirudi katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kuichezea Juventus kwa kipindi cha miaka minne, akitia saini dau la uhamisho lililovunja rekodi la £89m mwaka 2016.
Msimu uliopita , aliwachwa nje na Mourinho kwa awamu zote mbili za kombe la vilabu bingwa dhidi ya Sevilla
Lakini akapewa unahodha kwa mechi mbili za ligi ya Uingereza kuchukua mahala pake Antonio Valencia na amefunga magoli mawili kufikia sasa