Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 08.09.2018: Real Madrid, Liverpool, ManCity, Ramos, Salah, Fabinho, Terry, Leroy Sane, Rabiot

Ramos: Sikuwa na nia ya kumuumiza Mo Salah

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Real Madrid na Uhispania Sergio Ramos, 32, alisema kuwa hakutaka kumjeruhi mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 26 Mohamed Salah katika fainali ya kombe la vilabu bingwa na fikra zake ziko wazi alichofanya usiku huo. (Telegraph)

Mkufunzi wa Uingereza Gareth Southgate hana haraka ya kutia saini kandarasi mpya licha ya shirikisho la soka nchini humo FA kutaka kumpatia nyongeza muhimu ya mshahara. Mkataba wa Southgate unakamilika 2020. (Times - subscription required)

Southgate anafikiria kumchagua Marcus Rashford kwa mechi ya Jumamosi ya ligi ya kimataifa dhidi ya Uhispania -licha ya mshambuliaji huyo wa Manchester United , 20, kuanzishwa mechi moja pekee na timu yake kufikia sasa. (Mirror)

Beki wa Chelsea na Uingereza mwenye umri wa miaka 32 Gary Cahill huenda akaondoka klabu hiyo mnamo mwezi Januari iwapo hataorodheshwa katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Sun)

Adrien Rabiot wa PSG

Liverpool haina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na PSG Adrien Rabiot, 23, licha ya ripoti zilizomuhusisha na klabu hiyo ya Anfield na washindi hao wa ligue 1 mara nne. (Liverpool Echo)

Beki wa Tottenham na Ubelgiji Jan Vertonghen, 31, anatarajiwa kutia saini kandarasi ya mwaka mmoja katika mkataba wake ambao unakaribia kukamilika mwisho wa msimu huu. (Sun)

Leroy Sane

Sababu ya winga wa Manchester City Leroy Sane kuondoka katika kambi ya timu ya taifa ya Ujerumani kabla ya mechi dhidi ya Peru siku ya jumapili ni kwamba mpenzi wake anatarajiwa kujifungua. (Bild, via Mirror)

Beki wa zamani wa Chelsea na Uingereza John Terry, 37, anasema kuwa anataka kuendelea kucheza na amepokea maombi manne katika meza yake nchini Uingereza na ughaibuni. Terry aliyeichezea Aston Villa msimu uliopita atafanya uamuzi katika kipindi cha wiki mbili zijazo. (Mail)

John Terry

Barcelona na Chelsea zinamsaka kiungo wa kati wa Fulham na Uingereza ,15, Harvey Elliott, ambaye amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza wakati wa likizo ya mechi za kimataifa (London Evening Standard)

Birmingham City, ambao wako nambari 20 katika ligi ya mabingwa wakiwa na pointi nne hueda wakapokonywa pointi 12 kwa kukiuka sheria za matumizi katika kesi kubwa kuwahi kufanyika katika historia ya ligi hiyo ya Uingereza. (Telegraph)

Maelezo ya video,

Fatuma zarika asema mpinzani wake atapa kipigo

Manchester City wameipiku Chelsea na Tottenham katika kumsajili kipa wa Ireland ,16, Gavin Bazanu kutoka Shmirock Rovers.. (Sun)

Kipa wa Ubelgiji Thibaut Courtois

Kipa wa PSG na Ufaransa Alphonse Areola, 25, alitaka kuhamia Chelsea msimu uliopita ili kuchukua mahala pake kipa anayeondoka raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois, 26. (Le Figaro, via Express)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 24, amesema kuwa yuko tayari kucheza kwa mara ya kwanza katika ligi ya Uingereza bada ya kukosa kucheza mechi tangu aliposajiliwa kwa dau la £44m kutoka Monaco. (Sky Sports)

Mashabiki wa klabu ya Leicester City wanataka eneo moja la klabu hiyo kupewa jina la Claudio Ranieri, raia mtaliano aliyeiongoza timu hiyo kushinda taji la Uingereza 2016, mbali na sanamu yake kujengwa. (Leicester Mercury)

Claudio Ranieri

Mshambuliaji wa klabu ya Stoke City na Uhispania Bojan Krkic, 28, anatakiwa na mabingwa wa Serbia Red Star Belgrade, ambao wamewekwa pamoja na klabu ya Liverpool katika kombe la vilabu bingwa Ulaya. (Sport)

Klabu ya Girona nchini Uhispania imekubali mapendekezo ya kucheza mechi yao ya nyumbani dhidi ya Barcelona mjini Miami mnamo mwezi Januari.(Football Espana)

Mashabiki wa Girona watasafirishwa bure katika mechi hiyo, inayotarajiwa kuchezwa katika uwanja wa Miami Dolphins unaoweza kubeba watu' 65,000 kwa jina Hard Rock Stadium. (Guardian)