Manchester United: Kwa nini Jose Mourinho huhama klabu baada ya misimu mitatu?

Jose Mourinho

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho hajawahi kumaliza misimu minne katika klabu

Ubingwa mara mbili Ulaya, kushinda ligi mara nane na kutwaa vikombe vya ligi mara 15. Klabu zinazokuwa chini ya Mourinho hujua kushinda - lakini ni kwa nini Mreno huyo hung'atuka baada ya misimu mitatu klabuni?

Ni mara moja tu Mourinho alifika msimu wa nne kwenye klabu, lakini aliondoka Chelsea kabla ya Krismasi wakati wa kipindi chake cha kwanza huko Stamford Bridge.

Mourinho 55 amekuwa katika msimu wake wa tatu kama meneja wa Manchester United, klabu hiyo ilianza vibaya zaidi msimu katika kipindi cha miaka 29.

Walishindwa 3-1 na Liverpool wikendi na mwenyewe alikiri kwamba Liverpool walicheza vyema na walikuwa na ustadi kuwashinda United.

Kwa hivyo ni kipi husababisha Mourinho kuondoka klabuni baada ya misimu mitatu? Na kwa nini klabu zake kwa kawaida hufanya vibaya msimu wa tatu kuliko misimu miwili iliyotangualia. BBC inachunguza.

Vikombe alivyoshinda Mourinho misimu mitatu ya kwanza kwenye klabu

Maelezo ya picha,

Vikombe alivyoshinda Mourinho misimu mitatu ya kwanza kwenye klabu

Baada ya kuanza taaluma yake ya umeneja kwa kukaa kwa muda mfupi huko Benfica, Mourinho alifurahia matokeo mazuri akiwa na Uniao de Leiria hali iliyochangia Porto kumteua Mourinho ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 39 Januari 2002 kuwa meneja wao.

Porto:

 • 2001-02: Ilipanda kutoka nafasi ya tano katika ligi na kumaliza nafasi ya tatu baada ya kuchukua usukani Januari
 • 2002-03: Mabingwa wa Primeira Liga, washindi wa kombe la Uefa, washindi wa kombe la Ureno
 • 2003-04: Mabingwa wa Primeira Liga , washindi wa Ligi ya Mabingwa, washindi wa kombe la Ureno la Super Cup, ajiunga na Chelsea

Chelsea:

 • 2004-05: Mabingwa wa Ligi ya Premia, washindi wa Kombe la Ligi, Nusu fainali Ligi ya Mabingwa
 • 2005-06: Mabingwa wa Ligi ya Premia, washindi wa kombe la ngao ya jamii
 • 2006-07: Nafasi ya pili Ligi ya Premia, washindi wa kombe la FA, washindi wa Kombe la Ligi, nusu fainali Ligi wa Mabingwa
 • 2007-08: Aondoka kwa makubaliano mwezi Septemba

Inter Milan:

 • 2008-09: Mabingwa wa Serie A , washindi wa Supercoppa Italiana
 • 2009-10: Mabingwa wa Serie A , washindi wa Ligi ya Mabingwa, washindi wa Coppa Italia, ajiunga na Real Madrid

Real Madrid:

 • 2010-11: Mabingwa wa Copa del Rey, nafasi ya pili kombe La Liga, nusu fainali Ligi ya Mabingwa Ulaya
 • 2011-12: Mabingwa wa La Liga, fainali Ligi ya Mabingwa
 • 2012-13: Washindi wa Supercopa de Espana, nusu fainali Ligi ya Mabingwa, nafasi ya poli Copa del Rey. Aondoka Real kwa makubaliano

Chelsea:

 • 2013-14: Nafasi ya tatu Ligi ya Premia, nusu fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya
 • 2014-15: Mabingwa wa Ligi ya Premiea, washindi wa Kombe la Ligi
 • 2015-16:Aondoka Chelsea Desemba

Manchester United:

 • 2016-17: Mabingwa wa Europa League, washindi wa Kombe la Ligi, namba sita katika Ligi ya Premia
 • 2017-18: Nafasi ya pili Ligi ya Premia, nafasi ya pili Kombe la FA
 • 2018-19: United nafasi ya 10 baada ya mechi 7, wakiwa tayari wameshindwa mara tatu na wako nje ya kombe la Carabao

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mourinho alishinda ligi msimu wa kwanza Chelsea

Takwimu za ufanisi wake

Inaishia vipi?

Kuondoka Porto na mafanikio: Misimu miwili unusu baada ya kuchukua usukani, Mourinho aliondoka Porto baada ya kushinda ubingwa wa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na kushinda ligi ya nyumbani na kombe la ligi.

Chelsea, sehemu ya kwanza: Baada ya kushinda vikombe vyote vya nyumbani na kumaliza wa pili kwenye Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika msimu wake wa tata, droo ya 1-1 ya Septemba katika ligi ya mabingwa nyumbani kwa Rosenberg ilichangia kuondoka kwake msimu wa nne.

Inter: Mourinho aliondoka baada ya misimu miwili kuchukua usukani huko Real Madrid

Nafasu ya piki Real Madrid: Zikiwa zimebaki mechi mbili kabla ya kumalizika msimu ilitangazwa kuwa Mourinho angeondoka Real Madrid. Wakati huo kikosi chake kilikuwa nyuma ya Barcelona kwa pointi 13 na kupoteza kwa Atletico Madrid na kutupwa nje ya Ligi Mabingwa Ulaya kwenye nusu fainali.

Chelsea, kipindi cha pili: Mechi 16 za Ligi, mechi nne tu na pointi moja tu iliyobaki kushushwa daraja, muda wake Mourinho ulikuwa umefikia mwisho huko Chelsea kwa mara ya pili. Ndiye meneja aliyepata mafanikio zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Mikwaruzano na kukosana - nani wa kulaumiwa?

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mourinho alikosana na wachezaji wa Real Madrid baada ya kumuacha nje kipa Iker Casillas

Kuondoka kwa Mourinho huko Chelsea mara mbili na Real Madrid kulifuatia kukwaruzana na kukosana na maafisa na klabu hizo zote.

Ni kuwa mambo hugeuka wakati wa msimu wake wake wa tatu?

Porto: Aliondoka klabu akiwa shujaa.

Chelsea (mara ya kwanza): Uhusiano wa Mourinho na mmiliki Roman Abramovich uligeuka kuwa mbaya. Anaripotiwa kutofautiana na kutokuwepo pesa za kununua wachezaji. Avram Grant, alichukua mahala pake.

Inter: "Kama hujaongoza Real Madrid basi una kasoro kwenye taaluma yako," alisema Mourinho wakati akitangaza kuondoka Inter baada ya misimu miwili.

Real Madrid: "Hakuna mtu amefutwa," alisema rais wa Real Madrid Florentino Perez wakati akitangaza kuwa Mourinho ataondoka Bernabeu, lakini akitangaza hilo yalitokea majibizano na wachezaji wakuu klabuni.

Chelsea sehemu ya pili: Madaktari wa klabu walikumbana na hasira zake Mourinho msimu wake wa mwisho huko Stamford Bridge. Aliwakosoa kwa kuingia uwanjani kumpa huduma Eden Hazard wakati wa mechi iliyomalizika sare na Swansea.

Baada ya kupata kipigo kutoka kwa Leicester City, ambayo ilikuwa mechi ya mwisho ya Mourinho aliwakemea wachezaji wake;

Vita vya Mourinho msimu huu

Msimu huu, Mreno huyo amezozana na karibu kila mtu Old Trafford.

 • 29 Julai: Mourinho v aliwazomea mashabiki
 • 29 Julai: Mourinho v Ed Woodward - kuhusu ununuzi wa wachezaji
 • 10 Agosti: Woodward v Mourinho - alipozuiwa kuwasajili mabeki
 • 28 Agosti: Mourinho v wanahabari - alisema anastahili heshima
 • 1 Septemba: Mourinho v Anthony Martial - alisema yuko radhi Mfaransa huyo andoke
 • 24 Septemba: Paul Pogba v Mourinho Sura ya 1- Pogba azozana naye kwa kukosoa mbinu za klabu waliposhindwa na Wolves
 • 25 Septemba: Mourinho v Pogba Sura ya 2 - Apokonya Pogba unahodha
 • 26 Septemba: Mourinho v Pogba Sura ya 3 - Waonyesha wazi uhasama mazoezini