Mbwana Samatta: Kauli ya 'Haina Kufeli' imenifaa maishani na katika kandanda

Mbwana Samatta: Kauli ya 'Haina Kufeli' imenifaa maishani na katika kandanda

Jina la Mtanzania Mbwana Ally Samatta linagonga tena vichwa vya habari katika ulimwengu wa soka.

Baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi ya Ubelgiji na kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya KRC Genk ya Ubelgiji, na hivi sasa ripoti zinaeleza kuwa anatarajiwa kusajiliwa na klabu ya Aston Villa inayoshiriki ligi ya EPL.

Alianzaje na nini kilimpa msukumo wa kuendelea kujiboresha?

Samatta alibainisha majibu ya maswali hayo alipofanya mahojiano na mwandishi wa BBC Salim Kikeke mwaka 2018.