Tetesi za soka Ulaya: Nasri, Bailly, Mata, Bakambu, Wenger, Hernandez

Samir Nasri Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Samir Nasri alipigwa marufuku ya kucheza soka baada ya kugunduliwa kutumia dawa za kutitimuwa misuli

Everton inatafakari uhamisho wa aliyekuwa kiungo cha kati wa Arsenal na Manchester City Samir Nasri, mwenye umri wa miaka 31. Marufuku ya kutumia dawa za kutitimuwa misuli iliyomkabili mchezaji huyo raia wa Ufaransa inakamilika mwezi ujao. (Daily Mail)

Manchester United inataka kufanya mazungumzo mapya ya mkataba na Juan Mata mwezi huu. Mkataba wa mchezaji huyo wa miaka 30 wa kiungo cha kati raia wa Uhispania unamalizika msimu huu wa joto. (Sun)

Tottenham inatumai kumsajili mlinzi wa Manchester United na Ivory Coast Eric Bailly, mwenye miaka 24, mwezi Januari. (Daily Express)

Tottenham pia ina hamu ya kumsajili kiungo cha mbele wa Beijing Guoan - Cedric Bakambu. Guoan iliilipa Villarreal zaidi ya £ milioni 35 kwa mchezaji huyo wa miaka 27 kutoka Jamhuri a Kidemokrasi ya Congo mnamo Februari. (L'Est Republican, kupitiaTalksport)

Paris St-Germain inataka aliyekuwa meneja wa Arsenal - Arsene Wenger awe mkurugenzi wa soka wa timu hiyo. (RMC, kupitia Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paris St-Germain inamfukuzia Arsene Wenger kuwa mkurugenzi wake wa soka

Manchester United imewasilisha 'ombi la kutia kisunzi' kwa mlinzi wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa Lucas Hernandez. Mchezaji huyo mwenye miaka 22 ana thamani ya £ milioni 70, kifungu katika mkataba wake. (Marca, kupitia Metro)

Mlinzi wa Napoli Elseid Hysaj, mwenye miaka 24, alizuiwa kusaini mkataba na Chelsea msimu huu wa joto, kwa mujibu wa ajenti wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Albania. (Radio Kiss Kiss, kupitia Teamtalk)

Liverpool na Juventus wanatathmini mkataba wa Piotr Zielinski huko Napoli. Mchezaji huyo wa kiungo cha kati raia wa Poland mwenye miaka 24 yumo katika mzozo na klabu yake kuhusu kipengee cha kumuuza. (Calciomercato, kupitia Daily Mirror)

Barcelona tayari imeanza mpango wa kumsajili mlinzi raia wa Uholanzi wa timu ya Ajax Matthijs de Ligt, mwenye umri wa miaka 19. (Mundo Deportivo)

Mlinzi wa Italia Leonardo Bonucci, mwenye umri wa miaka 31, anasema uhamisho wake wa msimu mmoja wa £ milioni 40 kutoka Juventus kwenda AC Milan ulikuwa makosa makubwa yaliotokana na hasira. (Corriere dello Sport, kupitia Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paco Alcacer atasalia Borussia Dortmund

Mchezaji wa kiungo cha mbele wa Uhispania Paco Alcacer, mwenye umri wa miaka 25, atasalia Borussia Dortmund baada ya kukubaliana kusaini mkataba mpya.(Bild)

Tottenham inahamu ya kumsajili mlinzi wa Fiorentina na timu ya taifa ya Serbia Nikola Milenkovic, mwenye miaka 20. (Mirror)

Unaweza kuvutia na hii pia:

Newcastle scouts imemtazama mchezaji wa kiungo cha kati wa Olympiakos raia wa Guinea Mady Camara, mwenye miaka 21, wikendi iliyopita. (Sport in a Storm)

Arsenal na Manchester City zinatazamiwa kukosa kumsajili Cengiz Under, huku winga huyo mwenye miaka 21 raia wa Uturuki akitarajiwa kusaini mkataba mpya Roma. (Calciomercato)

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Cengiz Under anatarajiwa kusaini mkataba mpya Roma

Brentford inatarajiwa kutafuta meneja atakayeichukua nafasi ya kudumu ya Dean Smith ambaye ni meneja mpya wa Aston Villa wiki ijayo, lakini itatazama zaidi uzoefu katika ubingwa wakati wakitafuta mtu atakayeichukua nafasi hiyo.(Evening Standard)

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Brighton Steve Sidwell, mwenye miaka 35, ameanzisha duka lake la kuuza nguo za watoto baada ya kustaafu. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii