Tetesi za soka Ulaya: Milinkovic-Savic, Cahill, Allegri, Ghoulam, Ibrahimovic, Ake, Fabregas

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho
Image caption Meneja wa Manchester United Jose Mourinho

Jose Mourinho anataka Manchester United ifufue uhamisho wa Sergej Milinkovic-Savic Lazio baada ya ofa ya Euro milioni 80 dhidi ya kiungo huo wa kati wa Serbia kugonga mwamba msimu wa joto. (Sun)

Newcastle inatafakari uhamisho wa meneja wa Celtic Brendan Rodgers kuchukua nafasi ya Rafael Benitez katika uga wa at St James Park. (Mirror)

Manchester United imewasiliana na meneja wa Juventus Massimiliano Allegri huku tetesi kuhusu hatima ya Jose Mourinho uwanjani Old Trafford zikiendelea . (Calciomercato, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cahill, aliiongoza Chelsea kushinda kombe la FA msimu uliyopita

West Ham inawazia uhamisho wa mwezi Januari wa mlinzi wa Chelsea na England Gary Cahill,32, ambaye kandarasi yake inakamilika msimu wa joto. (Mirror)

Manchester United imetangaza ofa ya kumnunua beki wa kushoto wa Napoli na Algeria Faouzi Ghoulam, 27. (Calciomercato, via Manchester Evening News)

Mourinho pia anapania kumrudisha Manchester United, mshambulizi wa zamani wa Uswidi ambaye sasa anachezea LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37, mweiz Januari mwakani. (ESPN)

Kambi ya David de Gea , 27, ina matumaini kuwa kipa huyo wa Uhispania atatia saini kandarasi mpya na klabu ya Manchester United. (Manchester Evening News)

Atletico Madrid inammezea mate kiungo wa kati wa Chelsea na timu ya taifa ya Uhispania Cesc Fabregas, 31. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kiungo wa Chelsea na timu ya Taifa ya Hispania Cesc Fabregas 31 katikati

Kiungo wa kati wa Wales Ramsey asiruhusiwe kutoka Arsenal, hiyo ni kauli ya mshambulizi wa zamani wa klabu hiyo Alan Smith.

Ramsey, 27, ana chini ya mwaka mmoja kabla ya makataba wake na Gunners kumalizika. (Love Sport Radio)

Eric Bailly yuko tayari kufanya maamuzi yake ya siku zijazo wakati wa majira ya joto ikiwa ndoto yake kujiunga na Manchester United hayaitatimia.

Mlinzi huyo wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 24 ameaza michezo ya ligi tatu msimu huu. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mlinzi wa Manchester united anayetoka Ivory Coast Eric Bailly

Borussia Dortmund imeridhia mpango wa kumsajili Paco Alcacer kutoka Barcelona.

Mshamabulizi huyo wa miaka 25 wa timu ya taifa ya Uhispania yuko katika klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopo. (Bild - nchini Ujerumani)

Kiungo wa kati wa Real Madrid na Croatia Luka Modric, 33, ambaye anasemekana kuwa na "majonzi" katika uga wa Bernabeu anapigiwa upato kuhamia Inter Milan. (Gazzetta dello Sport, via Express)

Oleksandr Zinchenko atakuwa huru kuondoka Manchester City mwezi Januari.

Ajenti wa kiungo huyo wa kati wa Ukraine anatazamia kufufua uhamisho wake katika klabu ya Napoli. (Manchester Evening News)

Image caption Oleksandr Zinchenko kiungo wa kati wa Manchester Ciity

Mlinzi Darren Bent, ambaye aliachiliwa na Derby msimu huu wa joto, amesema yuko tayari kurejea kwa klabu yake zamani Ipswich.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England ambaye sasa ana miaka 34 kwanza alichezea timu ya Tractor Boys kati ya mwaka 2001-2005. (East Anglian Daily Times)

Manchester United inapigiwa upato kuzishinda vilabu vya Liverpool na Everton katika kinyang'anyiro cha kumsajili Isak Hansen-Aaroen,14, wa Norway. (Sun)

Mchezaji wa zamani wa Chelsea, Blackburn na Southampton Graeme le Saux anaamini meneja wa Manchester United Jose Mourinho anaweza kubaki Old Trafford kwa msimu wote. (Jersey Evening Post)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii