Mourinho azua vurugu baada ya Chelsea kusawazisha dhidi ya Man United Stamford Bridge

Mourinho akijaribu kumfuata mkufunzi wa kiufundi wa Chelsea baada ya ushindi wa Man United kupotea dakika ya lala salama

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho alizua vurugu katika eneo la touchline baada ya mshambuliaji wa Chelsea Ross Barkley kuizawazishia Chelsea katika dakika ya 96 na hivyobasi kuhifadhi matokeo mazuri ya kutoshindwa kwa timu yake tangu msimu mpya wa ligi ya Uingereza uanze.

Kikosi cha Mourinho kilionekana kupata ushindi wa 2-1 dhidi ya klabu yake ya zamani baada ya magoli mawili yaliofungwa na Anthony Martial kuisaidia Man United kutoka nyuma na kuongoza.

Chelsea ilikuwa imefunga bao lake kupitia Antonio Rudiger katika dakika ya 21.

Mourinho alikasirika sana baada ya Barkley kufunga katika dakika za lala salama kufuatia hatari katika goli la Man United hatua iliomfanya mkufunzi wa kiufundi wa Chelsea Marco Lanni kusherehekea mbele yake na kumkunjia ngumi katika eneo alilokuwa.

Raia huyo wa Ureno aliruka kutoka katika kiti chake kabla ya kushikwa na kuzuiliwa na baadhi ya maafisa wa Manchester United alipokuwa akijaribu kumfuata Lanni.

Mechi hiyo ilikamilika kwa mbwembwe huku Mourinho akiona ushindi wake ukichukuliwa mdomoni baada ya kuwaonyesha mashabiki wa Chelsea mataji matatu aliyoishindia timu hiyo alipokuwa mkufunzi wake.

Chelsea ilionekana kudhibiti mechi wakati Rudiger alipofunga bao kupitia kichwa baada ya Pogba kushindwa kumkaba vizuri kufuatia kona iliopigwa na Willian.

Hasira ya Mourinho

Mourinho alijaribu kuzuia hasira zake mchana wote wakati wa mechi hiyo aliporejea katika klabu aliyoifunza na kupata ufanisi mkubwa ikilinganishwa na klabu anayoifunza sasa ambapo anakabiliwa na shutuma nyingi.

Alisherehekea wakati Martial alipofunga bao lake la pili. Furaha yake isingeonekana iwapo isingechukuliwa na kamera.

Ni wakati huo ambapo muda ulipokuwa ukiyoyoma, hasira ya Mourinho iliongezeka na kumaliza mchezo kwa hali hiyo baada ya mkufunzi wa kiufundi wa Chelsea Lanni kusherehekea waziwazi huku akielekeza sherehe hiyo kwa Mourinho baada ya Barkley kusawazisha dakika za lala salama.

Hasira za mkufunzi huyo zilionekana kupanda hata kabla United kujaribu kulinda uongozi ambao unegwapatia ushindi muhimu, mbali na kwamba angeupata katika uwanja wa Stamford ambapo alishinda mataji matatu ya ligi .

Licha ya kujaribu kutulia ushindi huo ungekuwa muhimu sana kwa mkufunzi huyo.

Mada zinazohusiana