Majogoo wa jiji la Liverpool waibuka na ushindi wa 4-1 dhidi ya Cardiff city

liverpool

Chanzo cha picha, EPA

Mchezo uliokuwa unatazamiwa zaidi ni kati ya Liverpool dhidi ya Cardiff city ambapo majogoo wa jiji la Liverpool imeibuka na ushindi wa goli 4-1.

Magoli ya liverpool yamefungwa na Sadio Mane 2, Mohamed Salah 1, na Shaqiri amefunga goli 1.

Ushindi wa Liverpool unaipeleka timu hiyo kileleni mwa msimu kwa kujikusanyia alama 26 juu ya Manchester City ambayo ina alama 23 na itakuwa na mchezo siku ya Jumatatu dhidi ya Tottenham Hotspurs.

Matokeo ya michezo mingine

  • Watford wameshinda goli 3-0 dhidi ya Huddersfield Town
  • Fulham wakapata kipigo cha 3-0 dhidi ya AFC Bournemouth
  • Southampton wamekutana na wabishi Newcastle United na kutoshana nguvu ya bila bila
  • Brighton & Hove Albion imeshinda goli 1-0 dhidi ya Wolverhampton Wanderers

Mchezo utakaopigwa baadae ni kati ya Leicester City dhidi ya wagonga nyundo wa London West Ham United.

Kesho Jumapili kutakuwa na michezo mitatu Burnley itachuana na Chelsea 'The Blues' Crystal Palace watakuwa nyumbani kucheza na Arsenal, katika uwanja wa Old traford, Manchester United watacheza dhidi ya Everton.