Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 28.10.2018: De Jong, Conte, Allegri, Mata, Pogba, De Gea

Frenkie de Jong

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Frenkie de Jong

Manchester City huenda wakawapiku Tottenham katika kumwinda kiuungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21. (Daily Star Sunday)

Meneja wa zamani wa Chelsea manager Antonio Conte na kocha wa Juventus Max Allegri wametajwa kuwa wale wanaweza kuchukua nafasi yake Jose Mourinho kama meneja wa Manchester United mwaka ujao. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juan Mata

Arsenal watajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata ikiwa Mhispania huyo mwenye miaka 30 ataondoka bila mkataba msimu ujao. (Daily Star Sunday)

Juventus wanataka kumrudisha Paul Pogba kwenye klabu na watatoa ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 kiungo wa kati wa Manchester United mwezi January. (Tuttosport, via Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Paul Pogba

Manchester United wamemuamrisha Pogba aache kuzungumzia matatizo yake na meneja Jose Mourinho na uwezekano wake wa kuondoka Old Trafford. (Sunday Mirror)

West Ham wanatarajiwa kujiunga katika mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Atlanta United Miguel Almiron, mchezaji mwenye miaka 24 raia wa Paraguay kwa pauni milioni 25. (Football.London)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Miguel Almiron

Kocha mkuu wa Arsenal Raul Sanllehi anasema klabu hiyo haiwezi tena kuruhusu mikataba ya wachezaji wakuu kuingia mwaka wa mwisho. (Sunday Telegraph)

Napoli wamesema kuwa hawatasikiliza ofa zilizo chini ya pauni milioni 80 kwa mshambuliaji mwenye miaka 27 raia wa Italia Lorenzo Insigne anayehusishwa na Liverpool. (Gazetta dello Sport, via Inside Futbol)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Lorenzo Insigne

Aliyekuwa mchezaji wa Tottenham Ossie Ardiles anasema Muargentina mwenzake Mauricio Pochettino amepata ofa za kundoka klabu hiyo lakini hataki kuondoka. (Football.London)

Mchezaji wa zamani wa Manchester United Eric Cantona anasema anateseka kuona klabu yake ya zamani ikicheza chini ya usimamizi wake Jose Mourinho na angependa mchezaji wa zamani wa United kuchukua mahala pake. (Manchester Evening News)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Eric Cantona

Bora Kutoka Jumapili

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya England and Tottenham Dele Alli, 22 anakaribia kusaini mkataba mpya klabu hapo. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy, 31, amemkasirikia Meneja wake Claude Puel,ambaye anadaiwa kuwa alimuondoa kutomjumuisha mchezaji huyo katika mchezo leo jumamosi dhidi ya West Ham. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Dele Alli

Baadhi ya wachezaji wa Manchester United wanaweza kupigwa faini na klabu yao baada ya kukataa kuhudhuria hafla iliyoandaliwa na mfadhili wao ya kuandamana dhidi ya tatizo la usafiri ambao timu iliwahi kukabiliana nao katika mashindano ya ligi. (Mail)

Wakati huohuo Bosi wa United Jose Mourinho anataka wachezaji wake wajumuike naye kutembea kutoka Hotelini mpaka Uwanjani Old Traford kukwepa foleni inayoweza kutokea kama ilivyotokea kwenye mchezo dhidi ya Juventus kwenye UEFA ingawa watu wa usalama nchini humo wamepinga zoezi hilo. (Mail)

Mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 22, amekataa mkataba mpya aliopewa na Manchester United. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Malcom

Tottenham imepanga kumsainisha mchezaji wa Brazil Malcom, 21,wa Barcelona ambaye anahangaikia kuchukua nafasi ya Philippe Coutinho na Ousmane Dembele. (Corriere dello Sport - in Spanish)

Kiungo wa kati Mousa Dembele, 31 yuko katika orodha ya juu ya wachezaji wa Tottenham ambao meneja Mauricio Pochettino anataka kuwauza katika kipindi hiki cha kiangazi. (Sun)

Kiungo Aaron Ramsey, 27,amejihudhuru ili aondoke timu ya Arsenal katika kipindi cha kiangazi, ingawa amesema kuwa anashangaa kwanini Arsenal wamesitisha tena mkataba wake wa miaka minne (Evening Standard)