Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 29.10.2018: Lopetegui, Conte, Pochettino, Pogba, Kovacic, Benitez, Zielinski

Julen Lopetegui

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Julen Lopetegui

Real Madrid wanatarajiwa kumfuta meneja Julen Lopetegui leo Jumatatu na aliyekuwa meneja wa Chelsea Antonio Conte ateuliwe mara moja. (Marca)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola ameonya Real kuwa wana uwezekano mdogo wa kumchukua Mauricio Pochettino kutoka Tottenham kuchukua mahala pake Lopetegui. (Evening Standard)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mauricio Pochettino

Makamu wa rais wa Juventus Pavel Nedved amekana madai ya kumsaini tena kiungo wa kati wa Manchester United mfaransa Paul Pogba, 25. (Sky Italia, via Inside Futbol)

Manchester United na Chelsea wanatarajiwa kushindania kumsaini kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 27. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aaron Ramsey

Kiungo wa kati wa Chelsea raia wa Croatia Mateo Kovacic, 24, aliyekuwa kwenye mkopo kutoka Real Madrid anasema ni mapema sana kuzungumzia kuhama kabisa lakini anasema anafurahishwa sana na maisha ya London. (Evening Standard)

Newcastle wanaripotiwa kuwa tayati kumpa Rafa Benitez mkataba anaotaka - ikiwa anaweza kusubiri maombi fulani. (Newcastle Chronicle)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Rafa Benitez

Kiungo wa kati wa Poland Piotr Zielinski, 24, anayelengwa na Liverpool anatarajiwa kusaini mkataba mpya na Napoli. (Express)

Wafanyakazi kwenye uwanja wa Wembley walibaki na kazi nyingi ya ukarabati baada ya Philadelphia Eagles kucheza na Jacksonville Jaguars mechi ya NFL siku ya Jumapili chini ya saa 28 kabla la Tottenham kuialika Manchester City. (Mirror)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema kuna hatari ya kucheza huko Wembley baada ya mechi ya NFL kwenye uwanja huo huo. Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Marcus Rashford

Alliyekiuwa meneja wa Manchester United, West Brom na meneja wa Aston Villa Ron Atkinson, 79, anapata nafuu nyumbani baada ya siku kadhaa hospitalini kutokana na matatizo ya figo aliyopata akiwa likizoni huko Tenerife. (Birmingham Mail)

Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 21, hajawahi kufurahia kuwa mchezaji wa ziada hata wakati alikuwa na umri wa miaka mitano, kwa mujibu wa kocha wake wa zamani. (Mirror)

Bora Zaidi Kutoka Jumapili

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Frenkie de Jong

Manchester City huenda wakawapiku Tottenham katika kumwinda kiuungo wa kati wa Ajax Frenkie de Jong, 21. (Daily Star Sunday)

Meneja wa zamani wa Chelsea manager Antonio Conte na kocha wa Juventus Max Allegri wametajwa kuwa wale wanaweza kuchukua nafasi yake Jose Mourinho kama meneja wa Manchester United mwaka ujao. (Sunday Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juan Mata

Arsenal watajaribu kumsaini kiungo wa kati wa Manchester United Juan Mata ikiwa Mhispania huyo mwenye miaka 30 ataondoka bila mkataba msimu ujao. (Daily Star Sunday)

Juventus wanataka kumrudisha Paul Pogba kwenye klabu na watatoa ofa kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25 kiungo wa kati wa Manchester United mwezi January. (Tuttosport, via Mail on Sunday)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pogba

Manchester United wamemuamrisha Pogba aache kuzungumzia matatizo yake na meneja Jose Mourinho na uwezekano wake wa kuondoka Old Trafford. (Sunday Mirror)

West Ham wanatarajiwa kujiunga katika mbio za kumsaini kiungo wa kati wa Atlanta United Miguel Almiron, mchezaji mwenye miaka 24 raia wa Paraguay kwa pauni milioni 25. (Football.London)