Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 31.10.2018: Alexis Sanchez, Martinez, Mauricio Pochettino, Bale, Loris Karius, Neymar, Kylian Mbappe

Alexis Sanchez, 29,

Chanzo cha picha, PA

Klabu ya Paris St-Germain inapania kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, kutoka Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)

Meneja wa wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambaye pia amewahi kuongoza klabu ya Everton Roberto Martinez anapigiwa upatu kuwa meneja mpya wa kudumu wa Real Madrid. (Mail)

Wachezaji wa Tottenham wanahofia huenda meneja wao Mauricio Pochettino, ambaye amehusishwa na klabu za Real Madrid na Manchester United, akaondoka klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Telegraph)

Mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi kudai klabu hiyo ya Uturuki inataka mchezaji huyo wa miaka 25 kurejea kwenye klabu hiyo ya Merseyside mwezi Januari. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Michael Laudrup amekataa wito wa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Winga wa Wales Gareth Bale, 29, ameongoza kura ya mashabiki wa Real Madrid kuhusu mchezaji aliyefanya vibaya zaidi msimu huu. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Suso alipofunga mabao yake mawili ya kwanza katika klabu ya AC Milan

Chelsea inaazimia kumsajili Suso, mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool, mwezi Januari. (Express, kupitia Tutto Mercato Web)

Mshambuliaji wa Reiss Nelson, 18, ambaye yuko Hoffenheim kwa mkopo amepuuza madai kwamba huenda akaondoka klabu hiyo na kuhamia ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani. (Independent)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anatarajia klabu hiyo imnunulie mlinzi wa kati mwezi Januari wakati dirisha la uhamisho wa washezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)

Juventus ina mpango wa kumsajili mchezaji wa Colombia James Rodriguez mwezi Januari mwakani ikiwa Bayern Munich itaridhia kukatiza makubaliano ya kiungo huyo wa miaka 27 kutoka Real Madrid kwa mkopo. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Pierre-Emerick Aubameyang(kushoto)

Kuna tetesi kuwa mshambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang, 29, "alikosa kuhudhuria mkutano wa pamoja wa wachezaji au kukataa kushiriki mazoezi ya mwisho" kushinikiza uhamisho wake kutoka Borussia Dortmund hadi Gunners.

Hayo ni kwa mujibu wa meneja wa zamani wa klabu hiyo ya Ujerumani, Peter Stoger. (Mirror, via Bulinews)

Neymar, 26, amesema meneja wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel alikuwa sawa kuwaacha nje ya kikosi mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, na Adrien Rabiot, 23, wakati wa mechi dhidi ya Marseille baada ya wachezaji hao kuchelewa kufika kwa mkutano wa timu. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United ahaitamuajiri mkurugenzi kandanda hadi pale meneja Jose Mourinho atakapoidhinisha hatua hiyo. (ESPN)

Paul Mitchell ambaye ni Mkuu wa usajili na maendeleo katika klabu ya RB Leipzig, amesema hajawasiliana Manchester United kuhusu uwezekano yeye kupewa wadhifa wa mkurugenzi wa soka katika uga wa Old Trafford. (Manchester Evening News)

Mitchell pia anasema RB Leipzig inapania kumsajili mshambuliaji wa Everton forward Ademola Lookman, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopomsimu uliyopita. Hilo litafanyika endapo kiungo huyo wa miaka 21 ataamua kuondoka Goodison Park. (Sun)

Bora kutoka Jumanne

Besiktas wanataka kumrejesha kipa wa Liverpool Loris Karius kwa klabu hiyo ya Anfield. Kipa huyo alitia saini mkataba wa mkopo wa miaka miwili na klabu hiyo ya Uturuki.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Karius alifungwa mabao manne Europa League na KRC Genk

Wanataka Mjerumani huyo arejee Anfield mwezi januari na badala yake wakabidhiwe mshambuliaji Mbelgiji mwenye asili ya Kenya Divock Origi, 23. (90 Minutes)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mshambuliaji wa Ureno Cristiano Ronaldo, 33, amesema aliihama Real Madrid na kujiunga na Juventus kwa sababu rais wa klabu hiyo ya Uhispania Florentino Perez hakumfanya ajihisi kama mchezaji anayethaminiwa na kudhaminiwa sana. (L'Equipe, kupitia Express)

Mshambuliaji wa Barcelona anayechezea Ufaransa Ousmane Dembele huenda akaruhusiwa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. Chelsea, Liverpool na Arsenal ni miongoni mwa klabu ambazo zimehusishwa na kutaka kumchukua mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Sun)

Winga wa Lyon na Uholanzi aliyewahi kuichezea Manchester United Memphis Depay, 24, amedai kwamba hajajihisi kama mchezaji anayeheshimiwa. (ESPN)

Meneja Jose Mourinho ataungwa mkono Januari kuwanunua wachezaji zaidi kuimarisha kikosi cha Manchester United iwapo atawapata wachezaji wafaao. Inadaiwa kwamba ametengewa kitita cha karibu £100m. (Guardian)