Marco Ianni: Kocha wa Chelsea aliyemchokoza Mourinho aadhibiwa na FA

Jose Mourinho and Marco Ianni clash

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho na Marco Ianni walizua kituko baada ya Chelsea kusawazisha dhidi ya Manchester United dakika za mwisho

Mmoja wa makocha wa Chelsea Marco Ianni amepigwa faini na Chama cha Soka cha England (FA) kutokana na alivyosherehekea bao la dakika za mwisho la klabu yake dhidi ya Manchester United.

Chelsea walifunga bao dakika ya 96 na kusawazisha na matokeo yakawa 2-2 katika mechi hiyo ya Ligi ya Premia iliyochezewa uwanjani Stamford Bridge wiki moja iliyopita.

Ianni alitimka mbio na kusherehekea mbele ya benchi la kiufundi la Manchester United, jambo ambalo lilimkera sana Jose Mourinho ambaye aliwahi kuwa meneja wa Chelsea kwa vipindi viwili awali.

Mourinho alinyanyuka mbio kutoka kwenye kiti chake na kuonekana kutaka kumfukuza kwa hasira lakini akazuiwa na walinzi uwanjani.

FA wamesema Ianni amekiri kosa la "utovu wa nidhamu" na amepigwa faini ya £6,000.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jose Mourinho baada ya Marco Ianni kusherehekea mbele yake

Mourinho hakuadhibiwa na FA kutokana na mchango wake katika vurugu zilizotokea, lakini "amekumbushwa rasmi kuhusu wajibu na majukumu yake."

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Kocha wa Chelsea Marco Ianni akikimbia mbele ya benchi la kiufundi la Manchester United baada ya Ross Barkley kufunga bao la kusawazisha

Mreno huyo alisema Jumattau kwamba Ianni alimuomba radhi kwa tukio hilo lililotokea 20 Oktoba baadaye.

"Ningependa kuwashukuru Chelsea na [Maurizio Sarri - meneja wa sasa wa Chelsea]," Mourinho alisema.

"Kijana huyu mdogo hahitaji adhabu zaidi ya aliyoipata.

"Aliniomba radhi. Anahitaji kusamehewa - hastahili kufutwa. Alipitia tukio ambalo mwenyewe anakubali kwamba alikuwa amekosea..

"Natumai kwamba kila mtu atafanya hivyo na asivuruge taaluma na jamaa huyu mzuri sana. Pengine ni mtu mwenye matumaini makubwa sana katika kazi hii. Sitafurahia kamwe hatua zaidi ya hizo zikichukuliwa."

Baada ya mechi, Mourinho aliinua vidole vitatu, ambao ulionekana kuwa ujumbe wa kuwakumbusha mashabiki wa Chelsea kuhusu vikombe vitatu vya ubingwa wa ligi alivyoshinda akiwa na Chelsea 2005, 2006 na 2015.

Baada ya mechi kumalizika, Maurizio Sarri, alisema alizungumza na Mourinho na alikiri kwamba mkufunzi huyo wa Chelsea ndiye aliyekuwa na makosa.

Alisema alizungumza na mhusika na wakashughulikia tatizo hilo mara moja.

Baada