Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 01.11. 2018: Raheem Sterling, Foden, Malcom, Christian Eriksen, Aaron Ramsey, Ross Barkley

Raheem Sterling

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Raheem Sterling

Mshambuliaji wa Manchester City Raheem Sterling, 23, ambaye kandarasi yake inamalizika mwisho wa msimu huu, anatarajiwa kutia saini mkataba mpya hatua ambayo huenda ikatia kikomo shinikizo za mashabiki kutaka kiungo huyo kuondoka klabu hiyo kutokana na utenda kazi wake duni uwanjanani. (Manchester Evening News)

Aaron Ramsey, 27, kiungo wa kati wa Wales, ameambiwa na Arsenal anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Mail)

Borussia Dortmund inapania kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City na timu ya England ya wachezaji wa chini ya miaka 21 Phil Foden, 18. Huenda wakamnunua kwa kima cha euro 175,000. (Mail)

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte bado anapigiwa upatu kuchukua wadhifa wa kuwa mkufunzi mkuu katika klabu ya Real Madrid licha ya tetesi za mapema wiki hii kwamba hakuna uwezekano huo. (AS)

Arsenal na Tottenham wanang'ang'ania kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Malcom, 21, huku mchezaji huyo raia wa Brazil akinyimwa muda wa kucheza katika uwanja wa Nou Camp. (Mundo Deportivo kupitia Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Malcom,mshambuliaji wa Barcelona

Kiungo wa Kati wa Denmark Christian Eriksen, 26, anajiandaa kutia saini kandarasi ya kurefusha muda wake Tottenham. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Chelsea na England Ross Barkley, 24, huenda akawa "Frank Lampard mwingine", kwa mujibu wa mchezaji maarufu wa zamani wa klabu hiyo Pat Nevin. (Love Sport Radio)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Antonio Conte aliongoza Chelsea kushinda kombe la FA mwezi Mei

Juventus inatarajiwa kumwinda kiungo wa kati wa Manchester United kutoka Uhispania Juan Mata, 30 mwezi Januari.

Mata anahudumia mkondo wa mwisho wa kandarasi yake katika uga wa Old Trafford. (Evening Standard)

Manchester United ilikasirishwa na lugha chafu iliyotumiwa na kiungo wa kati wa Liverpool na England Jordan Henderson, 28, na wametumia hilo kujitetea kwenye rufaa yao kwa FA kumhusu meneja wake Jose Mourinho (Times)

Wolverhampton Wanderers imehusishwa na tetesi za kumtaka mshambuliaji Liverpool Divock Origi, 23, baada ya kuweka dau lake kwa mchezaji huyo raia wa Ubelgiji wakati wa msimu wa joto. (Birmingham Mail)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Brahim Diaz (kulia)

Mshambuliaji wa Manchester City na Uhispania U21 Brahim Diaz, 18, huenda akaondoka uga wa Etihad kuelekea Real Madrid. (Telegraph)

Rais wa zamani wa Uefa Michel Platini amesema kiungo wa kati wa Real Madrid na taimu ya taifa ya Ufaransa Raphael Varane, 25, yuko katika nafasi nzuri ya kushinda tuzo ya Ballon d'Or. (Marca)

Mshambulizi wa Manchester United na England Marcus Rashford amesherehekea siku yake ya kuzaliwa kwa kujumuika na watu wanaosherehekea Halloween. Rashford sasa ana miaka 21. (Manchester Evening News)

Bora kutoka Jumatano

Chanzo cha picha, PA

Klabu ya Paris St-Germain inapania kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, kutoka Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)

Mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi kudai klabu hiyo ya Uturuki inataka mchezaji huyo wa miaka 25 kurejea kwenye klabu hiyo ya Merseyside mwezi Januari. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Michael Laudrup amekataa wito wa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Winga wa Wales Gareth Bale, 29, ameongoza kura ya mashabiki wa Real Madrid kuhusu mchezaji aliyefanya vibaya zaidi msimu huu. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Karius alifungwa mabao manne Europa League na KRC Genk

Chelsea inaazimia kumsajili Suso, mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool, mwezi Januari. (Express, kupitia Tutto Mercato Web)

Mshambuliaji wa Reiss Nelson, 18, ambaye yuko Hoffenheim kwa mkopo amepuuza madai kwamba huenda akaondoka klabu hiyo na kuhamia ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani. (Independent)