Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 03.11.2018: Messi, Hazard, Pogba, Sarri, Diaz, Pochettino, Icardi

Pep Guardiola, Meneja wa Manchester City
Maelezo ya picha,

Pep Guardiola, Meneja wa Manchester City

Real Madrid inapania kumnunua kiungo wa kati wa Manchester City Brahim Diaz, 19. (Marca)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amepinga tetesi kwamba amekuwa akimshawishi mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 31, kujiunga na klabu hiyo. (Manchester Evening News)

Mshambuliaji wa Argentina Mauro Icardi, 25, inajiandaa kutia saini mkataba mpya na Inter Milan licha ya vilabu kadhaa vya Ulaya kummezea mate ikiwemo Chelsea. (Calcio Mercato - in Italian)

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amesema klabu hiyo haitamsajili mchezaji yeyote wakati wa msimu wa uhamisho wa wachezaji mwezi Januari. (Independent)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Nyota wa Chelsea Eden Hazard

Chelsea inataka kutumia fursa ya hali ya switafahamu ya inayokumba Real Madrid kuanzisha mazungumzo ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard.

Kiungo huyo wa miaka 27- huenda akapewa unahodha wa timu endapo atasalia katika ligi ya primia. (Telegraph)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino amedokeza azma yake ya kusalia katika klabu hiyo hadi atakapostaafu.(Football.London)

Pochettino amesema haamini kuwa wachezaji nyota wanajitolea kuimarisha klabu hiyo kwa sababu ya uwepo wake. (Sky Sports)

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri hana mpango wa kusajili tena kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 25. (Daily Mirror)

Chanzo cha picha, Reuters

Manchester United inataka kumsajili winga wa Fiorentina na Italiar Federico Chiesa, 21. (Calcio Mercato - Italian)

Mwanamuziki Sir Elton John - ambaye ni shabiki wa Watford- mwezi uliyopita alimtumia ujumbe mfupi mwenyekiti wa wa klabu hiyo Scott Duxbury kumuomba amsajili kipa wa Burnley na England Tom Heaton, 32. (Daily Mirror)

Lyon imekataa dau la euro milioni 44.8 la Manchester City la kumnunua kiungo wa kati wa UfaransaTanguy Ndombele, 21, wakati wa msimu wa joto. (RMC Sport - via City Watch)

Everton huenda ikafanya maamuzi kuhusiana na hatima ya siku zijazo za wilinzi wa Ufaransa Kurt Zouma, 24, na Ureno Andre Gomes, 25, ifikapo mwezi Januari mwakani. (Read Everton)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aaron Ramsey(kulia) alijiunga na Arsenal mwaka 2008

Kiungo wa kati wa Arsenal na Wales Aaron Ramsey, 27, huenda akakubali kujiunga na klabu yoyote ya Uingereza, kwa mujibu wa meneja wa timu yake ya taifa Ryan Giggs. (Sky Sports)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema hana mpango wa kumsajili kiunga hodari wa Arsenal kutoka Henrikh Mkhitaryan au mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, both 29, licha ya kufanya kazi nao katika klabu ya Borussia Dortmund. (Liverpool Echo)

Bora za Ijumaa

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Suarez amefunga mabao tisa dhidi ya Real Madrid

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick katika mechi ya El Clasico. (Sport 890, via Sun)

Liverpool inajiandaa kumpatia kandarasi mpya mlinzi wa England defender Joe Gomez, 21, miaka tatu na nusu hata kabla ya kumalizika kwa mkataba wake wa sasa. (Mirror)