Mazishi ya Vichai mmiliki wa Leicester City yaanza Thailand

Maua na picha za Vichai Srivaddhanaprabha ziliwekwa karibu na hekalu lake mjini Bangkok

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maua na picha za Vichai Srivaddhanaprabha ziliwekwa karibu na hekalu lake mjini Bangkok

mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.

Wanajeshi wa kifalme na jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha walishiriki katika maandamano makubwa ya kusherehekea maisha yake yaliyofanyika kabla ya mazishi yake huko Bangkok,

Wachezaji wa Leicester City wanatarajiwa kusafiri nchini Thailand kwa mazishi baada ya mechi yao dhidi ya Cardiff.

Bilionea Vichai alifariki pamoja na wafanyikazi wake wawili, rubani wa ndege aliyokua akisafiria na abiria mmoja baada ya ndege hiyo kuanguka muda mfupi baada ya kupaa.

Walioshuhudia wanasema ndege hiyo ilikuwa tu imemaliza kuondoka uwanjani pale ilipoanza kuyumba na kuanguka na kuwaka moto.

Jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Jamaa za Vichai Srivaddhanaprabha washiriki katika msafara wa wanajeshi kabla ya mazishi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Majeshi ya kifalme wakishiriki katika maandamano ya mazishi ya bwana Vichai

Mazishi yake yataanza na kafara ya kuoga ya waumini wa kibudha ambayo yatafuatiwa na sherehe ya siku saba ya kidini.

Mwandishi wa BBC Jonathan Head, mashariki mwa Asia ambaye anafuatilia sherehe hizo anasema kuwa zinafanywa faraghani,

Ndugu na jamaa zake wanatarajiwa kuwasili wwakati wowote kuazia sasa.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Waombolezaji wanaonekana kupitia milango ya vioo katika mazishi ya bwana Vichai

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Watu wa tabaka mbali mbali washiriki shughuli hiyo ya kupekee

Suala la hadhi ya mazishi ni muhimu sana nchini Thailand.

"Wakati wa mazishi haya utaona jinsi vito maalumu vitavyotolewa na mfalme Vajiralongkorn -

Pia amesema ''Watu watafuatilia kwa makini sana hii inaashiria jinsi Vichai alivyokua mashuhuri was.

"Alikua mwanabiasha maarufu, lakini zingine zilikumbwa na utata."

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Msafara wa mazishi ya Vichai Srivaddhanaprabha mjini Bankok

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha,

Vichai Srivaddhanaprabha aliinunua klabu ya Leicester City mwaka 2010

Mwili wa bwana Vichai uliwasili Thailand siku ya Ijumaa kabla ya mazishi yake .

Nusara Suknamai, Kaveporn Punpare, rubani Eric Swaffer na mpenzi wake, Izabela Roza Lechowicz, pia walifariki katika ajali hiyo ya ndege ya Jumamosi iliyopita.

Mabaki ya ndege hiyo iliondolewa nje ya uwanja siku ya Ijumaaa.

Uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo unaendelea.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Naibu waziri mkuu Prawit Wongsuwan akimwagia maji bustani la maua la Vichai Srivaddhanaprabha

Naibu wa waziri mkuu wa Thailand Prawit Wongsuwan,meneja wa timu ya soka ya wanawake ya Thailand na rais wa shirikisho la kandanda la Thailand ni miongoni mwa wageni wanaohudhuria mazishi hayo.

Kwa picha mazishi ya mmiliki wa klabu ya Leicester City aliyefariki kutokana na ajali ya ndege nje ya uwanja wa klabu hiyo nchini Uingereza yameanza kwao nchini Thailand.