Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 07.11.2018: Loftus-Cheek, Fifa, Welbeck, Wenger

Ruben Loftus-Cheek Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ruben Loftus-Cheek

Meneja wa Chelsea Maurizo Sarri amemzuia kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 22 kuhama kutoka West Ham mwezi Janauari. (Mirror)

Manchester City wanamtazama beki wa Crystal Place Wan-Bissaka, 20, wakati mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa England akiwa katika hali nzuri. (Mirror)

Wachezaji wa Leicester City wamewasili kwenye mazishi ya mmiliki wa klabu Thailand

Wasiwasi kuhusu De Bruyne Man City

Palace pia wanataka kutoaa ofa ya pauani milioni 10 kwa mchezaji wa Arsenal mwenye miaka 27 Danny Welbeck mwezi Januari. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Arsene Wenger amezitaja kuwa habari feki za kumuuzisha na klabua ya Seria A Milan. (beIN Sports)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United na Manchester City Leon Bailey, 21, anasema alikataa ofa ya Bayer Leverkusen kwa sababu hakutaka kufanya maamuzi ya haraka. (Manchester Evening News)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ameimbia Real Madrid kuwa hataondoka Spurs licha ya kupewa ofa ya paunia milioni 15 kwa mwaka kuchukua usimamizi wa klabua hiyo ya Uhispania. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mauricio Pochettino

Real Madrid wamefikia makubaliano kumsaini mchezaji wa miaka 20 kiungo wa kati wa Argentina Exequiel Palacios kutoka River Plate. (TeleMadrid - in Spanish)

Mshambuliaji wa England Jamie Vardy, 31, anaweka kwenye mnada kisanduku chake katika uwanja wa King Power kwa msaada kwa wakufu wa Vichai Srivaddhanaprabha. (Leicester Mercury)

Yafahamu majina ya timu za taifa Afrika na maana yake

Manchester City wa wamafikiria kiungo wa kati wa West Ham raia wa Ireland Declan Rice, 19, kuchukua mahala pake Fernandinho. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fernandinho

Bora zaidi kutoka Jumanne

Meneja wa zamani wa Arsenal Arsene Wenger yuko karibu kurejea usimamizi huko AC Milan. (France Football - in French)

AC Milan wana mpango wa kumuendea mlinzi wa Manchester United raia wa Ivory Coast Eric Bailly, 24, huku mchezaji huko akikasirishwa na ukosefu wa fursa chini ya umeneja wake Jose Mourinho huko Old Trafford. (ESPN)

Wachezaji wa Afrika waliomfaa Wenger huko Arsenal

Manchester City wanatafuta uwepo wa mshambuliajia wa Lille Nicolas Pepe, 23, huku mchezaji huyo raia wa Ivory akifunga mabao 8 msimu huu. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicolas Pepe

Meneja wa Southampton Mark Hughes atafutwa ikiwa Saints watakosa kuwashinda Watford siku ya Jumamosi huku Sam Allardyce na David Moyes wakitarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Mirror)

Mlinzi wa Argentina Pablo Zabaleta, 34, anatarajiwa kuundoka West Ham kuelekea Mashariki ya Kati. (Arab News)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United striker Zlatan Ibrahimovic, 37 ambaye sasa yuko na LA Galaxy anasema Ligi ya Premier imepewa hadhi ya juu bila sababu. (Four Four Two)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Mchezaji anayelengwa na Manchester United Leroy Sane, 22, anasema yuko upande mji mziuri, wakati wing'a huyo mjerumani akisema ana furaha huko Manchester City. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Senegal na Kasimpasa Mbaye Diagne, 27, analengwa na Wolves mwezi Januari. (Birmingham Mail)

Kipa wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 26, anasema hakuna mtu anahisi salama kung'ang'ania jesi nambari moja. (Evening Standard)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii