Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 08.11.2018: Conte, Llorente, Andersen, Pepe, Ibrahimovic, Anelka, Lozano

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antonio Conte

Aliyekuwa mkufunzi wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amekataa kufanya kikao na timu hiyo na anatishia kuwapeleka mahakamani kwa mshahara wake uliosalia, baada ya kufutwa kazi mwezi Julai huku akiwa amesalia na mwaka mmoja kabla ya kandarasi yake kukamilika. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Tottenham Fernando Llorente, 33, anasema atatumia fursa kurejea Uhispania baada ya kuwa na wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza huko Tottenham. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Fernando Llorente

Manchester United wanataka kumsaini mchezaji wa Sampdoria mwenye miaka 22 mlinzi raia wa Denmark Joachim Andersen. (La Republica, via Mirror)

Mexico wanafakiria kumteua meneja wa zamani wa Watford Quique Sanchez Flores kuwa meneja wao. (ESPN - in Spanish)

Southampton wanandaa pauni milioni 15 za kumsaini mshambuliaji wa Portimonense raia wa Japan Shoya Nakajima, 24. (Record, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicolas Pepe

Winga wa Lille Nicolas Pepe, 23, amekaribisha uvumi unaomhusisha na Arsenal na vilabu vingine vinavyoongoza Ulaya lakini anasisitiza kuwa ni mapema mno kupangia msimu ujao. (London Evening Standard)

Rais wa Fifa Gianni Infantino anasema kombe la dunia la mwaka 2022 nchini Qatar pia litaandaliwa na nchi majirani zake. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37, anasema hawezi kuhamia klabu ya Ulaya kwa mkopo wakati huu ambapo msimu wake huko MLS umekamilika. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Mlinzi wa zamani wa Tottenham Paul Miller ambaye sasa ni balozi wa klabu, anaamini kujengwa uwanja wa White Hart lane hakuwezi kukamilika kuandaa mechi za kwanza za timu hadi Februari. (Love Sport Radio)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Manchester City, Bolton na Chelsea Nicolas Anelka amekuwa kwenye mazungumzo na Lille kuhusu kuwa kocha wa timu yao ya vijana kwenye klabu hiyo ya Ufaransa. (L'Equipe - in French)

Brighton wanajadili kuhusu iwapo watamtoa kwa mkopo mchezaji wao mwenye miaka 18 Aaron Connolly mwezi Januari au kumpeleka kwenye klabu ya wachezaji walio chini ya miaka 23. (Argus)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicolas Anelka

Bora zaidi kutoka Jumatano

Meneja wa Chelsea Maurizo Sarri amemzuia kiungo wa kati wa England Ruben Loftus-Cheek, 22 kuhama kutoka West Ham mwezi Janauari. (Mirror)

Manchester City wanamtazama beki wa Crystal Place Wan-Bissaka, 20, wakati mchezaji huyo wa miaka 21 raia wa England akiwa katika hali nzuri. (Mirror)

Wachezaji wa Leicester City wamewasili kwenye mazishi ya mmiliki wa klabu Thailand

Palace pia wanataka kutoaa ofa ya pauani milioni 10 kwa mchezaji wa Arsenal mwenye miaka 27 Danny Welbeck mwezi Januari. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Arsene Wenger amezitaja kuwa habari feki za kumuuzisha na klabua ya Seria A Milan. (beIN Sports)

Mchezaji anayelengwa na Manchester United na Manchester City Leon Bailey, 21, anasema alikataa ofa ya Bayer Leverkusen kwa sababu hakutaka kufanya maamuzi ya haraka. (Manchester Evening News)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino ameimbia Real Madrid kuwa hataondoka Spurs licha ya kupewa ofa ya paunia milioni 15 kwa mwaka kuchukua usimamizi wa klabua hiyo ya Uhispania. (Sun)

Mada zinazohusiana