Juventus 1-2 Manchester United: Man United watoka nyuma na kufunga bao la lala salama mjini Turin

Juan Mata Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mkwaju wa adhabu uliopigwa na Juan Mata ulimwacha kipa wa zamai wa Arsenal Woljiech Kolscieny bila jibu

Manchester United iliishangaza Juventus kwa kufunga mabao mawili katika dakika tano za mwisho ili kuwashinda mabingwa wa Itali Juventus mjini Turin na kujipatia fursa muhimu ya kufuzu katika awamu ya muondoano ya kombe la vilabu bingwa Ulaya.

Juan Mata alifunga bao la mpira wa adhabu ikiwa imesalia dakika tano mechi kukamilika , kabla ya shambulio kali la Ashley Young kumgonga beki wa Juventus Alex Sandro na kuingia wavuni.

Christiano Ronaldo alikuwa amewaweka kifua mbele wenyeji kwa bao zuri dhidi ya klabu yake ya zamani.

Ronaldo alisubiri pasi ndefu ya Leonardo Bonucci kabla ya kumfunga kipa David De Gea na kuiweka miamba hiyo ya Itali kifua mbele ikiwa ni bao lake la kwanza katika michuano hiyo tangu ahamie klabu ya Itali.

Image caption Juan Mata

Juventus ilikuwa imegonga mwamba wa goli mara mbili kila kipindi cha mechi , huku Sami Khedira akigonga mwamba naye Paulo Dybala pia anaye akipiga mwamba.

Kikosi hicho cha Jose Mourinho hakikuonyesha mashambulizi yoyote na hata kushindwa kutishia katika lango la miamba hiyo ya Turin hadi mchezaji wa ziada Mata alipomfunga kipa wa zamani wa Arsenal Wojciech Szczesny kwa mkwaju mkali wa adhabu katika dakika ya 86.

Dakika tatu baadaye mkwaju mwengine wa adhabu uliopigwa na Young ulimgonga beki wa Juventus na kuingia wavuni.

Ushindi huo wa Man United unawaweka katika nafasi ya pili katika kundi H na pointi mbili juu ya Valencia ambao waliiwachapa Young Boys 3-1 katika mechi ya mapema huku ikiwa imesalia na mechi mbili.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Jose Mourinho alikabiliwa na beki wa Juventus :Leonardo Bonucci alipowapatia sikio mashabiki wa Juventus

United imekuwa na tabia ya kuimarika dakika za mwisho na kupata ushindi msimu huu, licha ya kwamba mkufunzi Jose Mourinho alisema kuwa klabu yake haina uwezo wa kufanya hivyo waliposhindwa na Juventus katika uwanja wa Old Trafford mwezi uliopita.

Lakini wakiweza kutoka nyuma na kupata ushindi dhidi ya Newvcastle na Bournemouth katika ligi ya Uingereza kuliwapatia afueni badala ya furaha na ushindi huu ulifufua kumbukumbu ya ushindi wa fainali ya kombe la vilabu bingwa dhidi ya Bayern Munich 1999.

Kikosi hicho cha Mourinho hakikuonyesha ari ya kuweza kushinda kombe hilo kama walivyofanya miaka 20 iliopita lakini, lakini tabia ya wachezaji wake wakati wa kipenga cha mwisho ilionyesha wazi umuhimu wa Man United kupata pointi tatu katika uwanja huo wa Turin.

Juventus ilikuwa imeshinda mechi zake tatu na walikuwa hawajafungwa katika michuano hiyo ya vilabu bingwa msimu huu kabla ya shambulizi hilo la Mata , ikiwa ni mara ya pili kwa Juventus kupoteza nyumbani katika awamu za muondoano ndani ya mechi 36.

United ambayo ilicheza bila mshambuliaji Romelu Lukaku ambaye pia hajulikani iwapo atacheza katika mechi ya Derby dhidi ya Manchester City siku ya Jumapili, ilimtumia Alexis Sanchez katika safu ya mashambulizi, lakini mchezaji huyo wa Chile alionekana kuwasaidia United katika kulinda lango badala ya safu ya mashambulizi.

Mchezo kama huo ulionekana kwa Anthony Martial ambaye alionekana akifukuzana na beki wa kulia wa Juventus Mattia De Sciglio ambapo United ililinda lango lake kabla ya Ronaldo kufunga bao lake.

Lakini United ambao walifanya mashambulizi matatu pekee walipohitajika watasonga mbele katika kundi hilo iwapo wataishinda Young Boys nyumbani baadaye mwezi huu huku Valencia ikishindwa kuilaza Juventus.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Cristiano Ronaldo alifunga bao lake la kwkanza katika mechi sita dhidi ya klabu yake ya zamani.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii