Arsenal vs Sporting 0-0: Gunners wafuzu kwa awamu ya mwisho ya kombe la Uropa

Danny Welbeck amebebwa kwa machela kutoka uwanjani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Welbeck amebebwa kwa machela kutoka uwanjani

Klabu ya Arsenal inahofia mshambuliaji wake Danny Welbeck aliumia vibaya wakati wa mechi yao dhidi ya Sporting Lisbon katika kombe la Uropa usiku wa Alhamisi

Mechi hiyo iliyochezewa katika uwanja wa Emirates iliisha bila bao lolote huku Gunners wakijinyakulia nafasi katika kundi la mwisho la timu 32.

Mechi hiyo hata hivyo iligubikwa na tukio la kuumia mguu kwa kiungo wa kimataifa wa England Danny Welbeck.

Meneja wa Arsenal Unai Emery amesema "yuko hospitali''. Tunasubiri matokeo ya uchunguzi wa kimatibabu, lakini tunahisi aliumia vibaya".

Emeri amesema kuwa kila jeraha ni tofauti, lakini huenda Welbeck amevujika sehemu fulani mguuni.

Welbeck aliumia katika dakika ya 25 ya mechi aliporuka na kuangukia vibaya mguu wake wa kulia.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kungo wa kati wa Arsenal Henrikh Mkhitaryan akiwa na Welbeck aliyeumia

Baadhi ya wachezaji wenzake waliathiriwa sana na ajali hiyo.

"Waliona kwamba ilikuwa ajali mbaya," aliongeza Emery.

"Mchezo wa soka huwa na ushindani mkubwa na ajali kama hizi hatuwezi kuepukana nazo, hungependelea itokee lakini ndio taaluma yetu."

Welbeck amefunga mabao tano msimu huu, pia alichezea England katika mechi yake dhidi ya Uhispania mwezi Septemba ambapo alishirikishwa katika kikosi cha Gareth Southgate.

Kikosi hicho kitacheza mechi ya kirafiki na Marekani pamoja na ligi ya mataifa dhidi ya Croatia.

Mlinzi wa zamani wa Arsenal Martin Keown, amabye sasa ni mchambuzi wa soka wa BT Sport, amesema: "Danny amehusika katika ajali kubwa mbiliakiwa uwanjani''

Aliongeza kuwa huenda mshambulizi huyo wa miaka 27 akaalia nje ya kikosi chake kwa muda.

Haki miliki ya picha Mesut Ozil
Image caption Mesut Ozil, ambaye hakushiriki mechi hiyo aliandika katika mtandao wake wa Twitter kumtakia Welbeck uponaji wa haraka

Takwimu ya mechi kati ya mahasimu hao wawili

  • Arsenal ilishindwa kufunga bao kwa mara ya pili chini ya ukufunzi wa Emery - pia walitoka sare dhidi ya Manchester City katika mchezo wao wa kwanza na meneja huyo wa Uhispania
  • Sporting ilishindwa kufunga bao la moja kwa moja katika mechi zao zote mbili dhidi ya Gunners msimu huu.
  • Kando na kufuzu, Arsenal imefanikiwa kumaliza mechi ya makundi mara tatu mfululizo bila kufungwa katika michuano ya ligi ya mabingwa tangu mwaka 2007-08.
  • Sporting iliweza kufanya hivyo katika michuano ya ligi ya Uropatangu Septemba 2011 ilipofunga (2-0 didhi ya FC Zurich).
  • Aubameyang alishindwa kufunga mabao ya wazi zaidi ya mara mbili ikilinganishwa na wachezaji wengine wa Arsenal (mara nne).

Henrikh Mkhitaryan (Arsenal) alitajwa kuwa mchezaji bora wa siku

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Henrikh Mkhitaryan katika mechi ya Arsenal dhidi ya Sporting Lisbon

Meneja wa Arsenal Emery alisema: "Kila mechi tunataka mchezo mzuri kutoka kwa kila mchezaji''.

Aliongeza kuwa Sporting ni timu kubwa, na wachaziji wake wamemakinika. '' Kwa hivyo tulihitaji kuwa waangalifu sana.

Arsenal wanarejea uwanjani tena Jumapili hii katika mchuano wa ligi ya primia watakapokutana na Wolves (16:30 GMT).

Gunners watacheza tena katika ligi ya Uropa Novemba 29 November, ambapo watakuwa wenyeji wa Vorskla Poltava huku Sporting wakichuana dhidi ya Qarabag siku hiyo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii