Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 13.11.2018: Matic, Nasri, Conte, De Bruyne, Dembele, Solari, Alves, Welbeck

Jose Mourinho Haki miliki ya picha Getty Images

Hatua ya meneja wa Manchester United Jose Mourinho kumchagua kiungo wa kati Nemanja Matic,30, imeendelea kuzua maswali miongoni mwa baadhi ya wachezaji wenzake wa kimataifa kutoka Serbia. (Times - subscription required)

Mpango wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Ufaransa Samir Nasri kuhamia West Ham uko mashakani kufuatia hali ya kiafya ya kiungo huyu wa miaka 31. (Daily Mirror)

Santiago Solari anatarajiwa kuteuliwa meneja wa Real Madrid kwa mkataba utakaoendelea hadi mwisho wa msimu ujao. (Marca - in Spanish)

Kiungo wa kati wa Tottenham na Ubelgiji Mousa Dembele amesafiri nchini Qatar kwa matibabu maalum ya kifundo cha mguu . (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Dembele alijiunga na Spurs mwaka 2012

Aliyekuwa meneja wa Chelsea Antonio Conte anasema atasubiri hadi msimu wa joto kuanza kazi yake mpya . (Rai Sport, via Goal)

Uamuzi wa Conte kusubiri inamaanisha Chelsea huenda ikamlipa euro milioni 11 kama fidia - hii ikiwa inajumuisha pesa zote alizokuwa alipwe meneja huyo katika mwaka wa mwisho wa mkataba wake. (Daily Mirror)

Vilabu vinavyoshiriki ligi ya primia vitaruhusiwa kuwasajili wachezaji 12 wa ulaya katika vikosi vyaovya wachezaji 25 chini ya kanuni mpya ya shirikisho la soka linapojiandaa katika mpango wa Uingereza kujiondoa kutoka Muungano wa Ulayo mchakato naofahamika kama Brexit. (Times)

Image caption Antonio Conte amesema atasubiri hadi msimu wa joto kuanza kazi yake mpya

Vilabu vya Borussia Dortmund na Marseille vinapania kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal Ben Cottrell, alaiye na umri wa miaka 17.(Sun)

Beki wa Paris St-Germain Dani Alves,35, amesema amedokeza azma yake ya kucheza ligi ya primia kabla astaafu. (Daily Telegraph)

Meneja wa Arsenal Unai Emery na wachezaji wake walizungumza na mshambuliaji wa Gunners na England aliyeumia Danny Welbeck katika ujumbe wa video kabla ya mechi yao ya Jumapili dhidi ya Wolves ambapo walitoka sare ya bao 1-1. (Guardian)

Kungo wa kati na mshambuliaji hodari wa Manchester City Kevin de Bruyne anatazamiwa kurejea uwanjani mapema kuliko ilivyotarajiwa baada ya kupona goti lake. (Guardian)

Haki miliki ya picha Rex Features

Brighton inatarajiwa kukata rufaa ya kupinga kadi nyekundi iliyopewa kiungo wake wa kati Dale Stephen katika mechi ya siku ya siku ya Jumamosi ambapo waliinyuka Cardiff mabao 2-1. (Argus)

Klabu ya Al-Jazira kutoka Milki ya Kiarabu UAE inapania kumteua Michael Reiziger kama kocha wake.

Reiziger ambaye alikuwa mlinzi wa zamani wa Ajax, Barcelona na Middlesbrough kwa sasa anasimamia wachezaji wa ziada wa Ajax. (De Telegraaf - in Dutch)

Bora katoka Jumatatu

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema amemkabili mchezaji wa kiungo cha mbele wa timu hiyo Raheem Sterling baada ya ushindi wa 3-1 katika mechi ya derby dhidi ya Manchester United kwasababu ya kujionyesha au kujigamba kwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 katika dakika za mwisho za mechi. (Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Pep Guardiola

Everton, Newcastle na West Ham zinataka kumsajili mchezaji raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 28 Yacine Brahimi, ambaye kandarasi yake na Porto inamalizika msimu ujao wa joto. (Sun)

Huenda Manchester City wasipokewe vyema Alhamisi wakati wakurugenzi wakuu wa tim katika ligi kuu England watakapokutana kufuatia tuhuma kuhusu matumizi ya fedha katika klabu hiyo. (Times - subscription required)

Winga wa Bayern Munich Franck Ribery, mwenye umri wa miaka 35, alijibizana na mwandishi wa Ufaransa baada ya timu yake kufungwa 3-2 na Borussia Dortmund Jumamosi. (Bild, via Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Franck Ribery alijiunga na Bayern Munich mwaka 2007

Everton wana wasiwasi kuhusu kujeruhiwa kwa mchezaji wa miaka 29 Gylfi Sigurdsson, aliyeondoka Stamford Bridge akiwa amevaa kiatu cha matibabu baada ya kupigwa chenga na mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Jorginho katika mechi iliyomalizika kwa sare kati ya pande hizo mbili. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii