Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi 22.11.2018: Neymar, Pogba, Skriniar, Smalling, Guardiola, Mourinho

Milan Skriniar Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Milan Skriniar

Chelsea wamejiunga kwenye mbio za Manchester United kumsaini mchezaji wa Inter Milan anayewekewa thamani ya pauni milioni 70 mlinzi raia wa Slovakia Milan Skriniar, 23. (Sun)

Manchester United watataka kumsaini mlinzi wa Fiorentina na Serbia Nikola Milenkovic, 21, mwezi Januari (Sky Sports)

Wakati wanataka kuwasaini walinzi, Manchester United pia wamezungumza kuhusu mkataba na beki wa England Chris Smalling, 29. (Mail)

Nahodha wa zamani wa Manchester United Paul Ince anasema itafaidi pande zote ikiwa kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 25, ataondoka Januari. (Paddy Power, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anahisi huenda akaongoza kandanda ya kimataifa hivi karibuni. (Telegraph - subscription required)

Barcelona wanataka mshambulizi raia wa Brazil Neymar, 26, kumaliza uwepo wake huko Paris St-Germain na kutafuta njia ya kurudi huko Nou Camp. (Goal)

Kiungo wa kati wa Stoke Charlie Adam, 32, hajakana kurudi Rangers kujiunga na mchezaji mwenzake huko Liverpool Steven Gerrard. (Talksport, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Wing'a wa miaka 20 wa Borussia raia wa Marekani Christian Pulisic amehusishwa na kuhama kwenda Liverpool na anaamini kuwa meneja Jurgen Klopp na meneja ambaye wachezaji wote wangependa kumchezea. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Uingereza Dwight Gayle, 28, anafuta mkataba wa kudumu kwenda West Brom msimu ujao. (Northern Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Divock Origi

Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Ubelgiji Divock Origi, 23, na mlinzi wa zamani wa Cameroon Joel Matip, 27, watahamia Uturuki mwezi Januari. Galatasaray wanamtaka Origi huku Matip akilengwa na Fernerbahce.

Kuhama kwa mchezaji wa miaka 20 wa River Plate kiungo wa kati raia wa Argentina Exequiel Palacios kwenda Real Madrid kwa kima cha pauni milioni 22.3 kutathibitishwa baada ya fainali za Copa Libertadores (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Beki wa Manchester City Mfaransa Aymeric Laporte anasema atahitaji kuwa katika kiwango cha Sergio Ramos wa Real Madrid ili kutajwa kuwa mlinzi bora zaidi duniani. (Evening Standard)

Didier Drogba anaaminia meneja wake wa zamani huko Chelsea Jose Mourinho angeshinda mataji mara mbili au tatu ikiwa angeongoza Manchester City badala ya majirani Manchester United. (Mirror)

Mshambuliaji wa zamani wa Ireland Tony Cascarino anaamini Mick McCartht yuko tayari kuchukua mahala pake Martin O'Neill kama meneja wa timu ya taifa. (Talksport)

Mada zinazohusiana