Tetesi za soka Ulaya Ijumaa 23.11.18: Rashford, Bolt, Neves, Eriksen, Heaton, Wagner, Almiron

Marcus Rashford Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcus Rashford yupo tayari kujadiliana na Real Madrid, asipojumuishwa katika orodha ya kwanza ya Manchester United

Mshambuliaji wa England Marcus Rashford, mwenye umri wa miaka 21, yupo tayari kujadiliana na Real Madrid iwapo hatofanikiwa kujumuishwa katika orodha ya kwanza ya timu ya Manchester United. (Sun)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema hana wasiwasi kuhusu mkataba wa Christian Eriksen na anasisitiza klabu hiyo 'inawajibika' kumpatia mchezaji huyo wa kiungo cha kati raia wa Denmark mkataba mpya wa muda mrefu. (Standard)

Timu ya kiwango cha juu ya Uturuki Sivasspor imewasiliana na mshindi mara nane wa mbio fupi katika Olimpiki, Usain Bolt katika kinachowezekana kuwa ni mkataba wa nusu ya pili katika msimu.(TRT World)

Manchester United inaamini Jose Mourinho ameepuka uasi wa wachezaji Old Trafford. (Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Je Ruben Neves ataelekea Juventus?

Juventus inatafakari kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Wolves na timu ya taifa ya Ureno, Ruben Neves, mwenye umri wa miaka 21, ifikapo Januari. (Tuttosport)

Manchester United inatuma maafisa kwenda kumwinda mlinzi wa Fiorentina Nikola Milenkovic, mwenye miaka 21, atakapocheza dhidi ya Bologna Jumapili. (Mail)

Mkuu wa Newcastle Rafa Benitez anataka kumsajili mshambuliaji wa Atlanta United Miguel Almiron. West Ham na Everton pia wana hamu ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Paraguay mwenye thamani ya £15m. (Sun)

Kocha mkuu wa Watford Javi Gracia atasaini mkataba mpya katika klabu hiyo wiki ijayo utakaomfikisha hadi mwisho wa kampeni ya mwaka 2020-21. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Huenda Mo Salah akaondoka Liverpool "katika msimu mmoja au miwili" kwa mujibu wa kocha wa Misri

Winga Mohamed Salah, mwenye umri wa miaka 26, huenda akaondoka Liverpool "katika msimu mmoja au miwili" iwapo klabu hiyo itashindwa kunyanyua taji, kwa mujibu wa kocha wa Misri Javier Aguirre. (ONSport kupitia Goal.com)

Kipa wa Burnley na timu ya taifa England Tom Heaton, mwenye miaka 32, ana hamu ya kuhamia Leeds United. (Talksport)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Inter Milan Radja Nainggolan, mwenye umri wa miaka 30, amesema hana majuto kuhusu kukataa uhamisho kwenda katika ligi kuu England. Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Ubelgiji alihusishwa na uhamisho kwenda Chelsea na Manchester United. (ESPN)

Haki miliki ya picha EPA

Crystal Palace na West Ham wana hamu ya kumsajili mchezaji mwenye umri wa miaka 30 wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ujerumani Sandro Wagner, lakini timu hizo mbili katika ligi ya Primia zinakabiliwa na ushindani kutoka Galatasaray na klabu nyingine katika ligi ya Ujerumani Bundesliga. (Bild)

AC Milan ina hamu ya kumsajili beki wa kati wa Atletico Madrid na mchezaji timu ya taifa ya Uruguay Diego Godin, ambaye yupo huru katika msimu wa joto ujao.(Corriere dello Sport)

Aliyekuwa mchezaji wa kiungo cha kati wa England Scott Parker, mwenye umri wa miaka 38, atakuwa naibu meneja wa Claudio Ranieri huko Fulham. (Football.London)

Stoke inapanga uhamisho wenye thamani ya £5m kwa mshambuliaji mwenye umri wa miaka 22 wa Birmingham Che Adams ifikapo Januari. (Telegraph)

Aston Villa inatafakari kumuita kwa mara nyingine kipa wa England Jed Steer, mwenye miaka 26, kutoka mkataba wake wa mkopo huko Charlton Athletic ifikapo Januari. (Birmingham Mail)

Bora za Alhamisi

Nahodha wa zamani wa Manchester United Paul Ince anasema itafaidi pande zote ikiwa kiungo wa kati Mfaransa Paul Pogba, 25, ataondoka Januari. (Paddy Power, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anahisi huenda akaongoza kandanda ya kimataifa hivi karibuni. (Telegraph - subscription required)

Barcelona wanataka mshambulizi raia wa Brazil Neymar, 26, kumaliza uwepo wake huko Paris St-Germain na kutafuta njia ya kurudi huko Nou Camp. (Goal)

Kiungo wa kati wa Stoke Charlie Adam, 32, hajakana kurudi Rangers kujiunga na mchezaji mwenzake huko Liverpool Steven Gerrard. (Talksport, via Express)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar

Wing'a wa miaka 20 wa Borussia raia wa Marekani Christian Pulisic amehusishwa na kuhama kwenda Liverpool na anaamini kuwa meneja Jurgen Klopp na meneja ambaye wachezaji wote wangependa kumchezea. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Newcastle United raia wa Uingereza Dwight Gayle, 28, anafuta mkataba wa kudumu kwenda West Brom msimu ujao. (Northern Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Divock Origi

Mshambuliaji wa Liverpool raia wa Ubelgiji Divock Origi, 23, na mlinzi wa zamani wa Cameroon Joel Matip, 27, watahamia Uturuki mwezi Januari. Galatasaray wanamtaka Origi huku Matip akilengwa na Fernerbahce.

Kuhama kwa mchezaji wa miaka 20 wa River Plate kiungo wa kati raia wa Argentina Exequiel Palacios kwenda Real Madrid kwa kima cha pauni milioni 22.3 kutathibitishwa baada ya fainali za Copa Libertadores (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jose Mourinho

Beki wa Manchester City Mfaransa Aymeric Laporte anasema atahitaji kuwa katika kiwango cha Sergio Ramos wa Real Madrid ili kutajwa kuwa mlinzi bora zaidi duniani. (Evening Standard)

Didier Drogba anaaminia meneja wake wa zamani huko Chelsea Jose Mourinho angeshinda mataji mara mbili au tatu ikiwa angeongoza Manchester City badala ya majirani Manchester

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii