Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 25.11.2018: De Gea, Pogba, Benitez, Hazard, Hughes, Neves

David de Gea Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David de Gea

Kipa wa Manchester United David de Gea atajiunga na Paris St-Germain msimu ujao wakati mkataba wa mchezaji huyo mwenye miaka 28 raia wa Uhispania utakamilika huko Old Trafford. (Mail on Sunday)

Jeventus itakabiliwa na changamoto katika jitihada za kumpa ofa Paul Pogba huku Inter Milan nayo ikitaka kutoa ofa yake kwa kiungo huyo wa kati mfaransa. (Tuttosport - in Italian)

Inter Milan wanaweza kumpa meneja Jose Mourinho wachezaji ambao amekuwa akiwatafuta kwa muda mrefu - mlinzi raia wa Slovekia Milan Skriniar, 23, na wing'a raia wa Croatia Ivan Perisic kama sehemu ya makubaliano. (Sunday Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba

Meneja wa Newcatsle Rafael Benitez anatafutwa na klabu ya China ya Guangzhou Evergrande. Mhispania huyo yuko mwaka wake wa mwisho huko St James's Park. (Sun on Sunday)

Kipa wa Columbus Crew na Marekani, Zack Steffen, 23, ataletwa na Manchester City kama kipa wa ziada wa raia wa Brazil Ederson, 25. (Sun on Sunday)

Guardiola anasema kiungo wa kati wa Brazil Fernandinho, 33, atapumzishwa wakati wa shughuli nyingi za City za msimu huu. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Chelsea wanaamini mshambualiaji Mbelgiji Eden Hazard ataondoka Stamford Bridge, na tayari wameanza kujipanga na kutokuwepo kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (OK Diario - in Spanish)

Meneja wa Southampton Mark Hughes anasema kelele kutoka kwa mashabiki wa Saints kuhusu hatma yake klabuni wakati wa kushindwa kwa mabao 3-2 na Fulham zilitabiriwa. (Mail on Sunday)

Mshambuliaji wa AC Milan raia wa Argentina Gonzalo Higuain, 30, huenda akarudi Juventus mwisho wa msimu. Mchezaji huyo wa miaka 30 alihama kwa mkopo mwezi Agosti lakini wasiwasi kuhusu bajeti unamaana kuwa Milan hawawezi kulipa pauni milioni 32 kuufanya mkataba uwe wa kudumu. (Corriere dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Naye mchezaji wa miaka 37 raia wa Sweden Zlatan Ibrahimovic huena akajiunga na Milan kwa mkopo kwa miezi sita kutoka Los Angeles Galaxy.(Gazetta dello Sport, via Football Italia)

Kiungo wa kati wa Manchester United raia wa Uhispania Juan Mata, 30, anatarajiwa kupewa mkataba mpya wa miaka mitatu kusalia Old Trafford kufuatia dalili kutoka Atletico Madrid. (Daily Star Sunday)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eliaquim Mangala

Inter Milan na Wolves wanataka kumsaini kiungo wa kati Mfaransa wa Manchester City Eliaquim Mangala, 27, msimu uajo. (Sun on Sunday)

Wolves pi wanataka kumwendea wing'a wa Monaco Keita Balde, aliye kwenye mkopo huko Inter Milan lakini West Ham pia wanammezea mate mchezaji huyo wa miaka 23 raia wa Senegal. (Birmingham Mail)

Mada zinazohusiana