Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 27.11.2018: Wenger, Cahill, Ibrahimovic, Arnautovic, Witsel, Pulisic

Arsene Wenger Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kurejea kwenye usimamizi wa kandanda huko Bayern Munich ambao wanamuona Mfaransa huyo kama mrithi wa Nico Kovac. (Telegraph)

AC Milan wamekataa fursa ya kumsaini beki wa Chelsea na England Garry Cahil, 32. (Calciomercato, via Talksport)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso hajakana uwezekano wa kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37. (Sun)

Mshambualia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema Chelsea wanalenga nafasi nne za kwanza msimu huu na hawatakuwa mabingwa. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Manchester United wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Ham na Austria Marko Arnautovic, 29. (Telegraph)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefufua mikakati zake kumwinda mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ubelgiji Axel Witsel. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Moyes

Meneja wa zamani wa Manchester United David Moyes anaamini angepewa muda zaidi huko Old Traffor. (Talksport)

Borussia Dortmund wanajiandaa kumuuza wing'a Mmarekani Christian Pulisic kwenda Chelsea au Liverpool kwa pauni milioni 70 ikiwa mchezaji huyo wa miaka 20 atakaa Ujerumani hadi msimu ujao. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Declan Rice

West Ham wanajiandaa kusubiri hadi msimu ujao kabla ya kuanza mazungumzo ya mkataba na mlinzi raia wa Jamhuri ya Ireland Declan Rice, 19. (Guardian)

Mchezaji wa kimataifa raia wa England Peter Beardsley anafunza klabu isiyo katika Ligi ya Gateshead kufuatia kutimuliwa kwake kama naibu meneja wa Newcastle mwezi January. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Tanguy Ndombele

Everton wanammezea mate kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Tanguy Ndombele, 21, lakini anakabiliwa na ushindani kutoka Manchester City. (Liverpool Echo)

Arsenal wanamwinda beki wa Galatasaray Ozan Kabak lakini mchezaji huyo wa miaka 18 pia anawindwa na Inter Milan. (Sabah, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ozan Kabak

Klabu ya Serie A wanataka kumsaini beki wa Chelsea Mnigeria Ola Aina kwa mkataba wa kudumu baada ya kufurahishwa na mchezaji huyo tangu awasili kwa mkopo msimu huu. (Goal)

Inter Milan wanaripotiwa kutoa ofa kwa kwa mlinzi wa Manchester City na Ufaransa Eliaquim Mangala, 27. (Football Italia, via Talksport)

Bora Kutoka Jumatatu

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmane Dembele

Mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, ameomba kuondoka Barcelona mwezi Januari na kuondoka kwake kutamruhusu Neymar kurudi Nou Camp kutoka Paris St-Germain. (Goal)

Mshambuliaji wa Chelsea Eden Hazard, 27 amekana kuwa atahamia Paris St-Germain, lakini amekiri kuwa ataondoka Stamford Bridge msimu huu. (Canal+ via Goal)

Mkurugenzi wa Milan Leonardo ameripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Chelsea kuhusu kiungo wa kati Cesc Fabregas, 31, na walinzi Gary Cahill, 32, na Andreas Christensen, 22. (Football Italia)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lorenzo Pellegrini

Manchester United ilituma maajenti kumtazama kijana mlinzi wa West Ham Declan Rice, 19, wakati Hammers walishindwa kwa mabao 4-0 na Manchester City siku ya Jumamosi. (Metro)

Beki wa Barcelona Jordi Alba, 29, amekiri kuwa hajapewa mkataba mpya klabuni na kuacha hatma yake gizani. (ESPN)

Manchester United wanaweza kungoja kumsaini kiungo wa kati wa Roma Lorenzo Pellegrini baada ya kugundua kuwa kupengee cha kuuvunja mkataba wake kinaweza kutumiwa mwisho wa msimu. (Mirror via Manchester Evening News)