Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 28.11.2018; Cole, Wenger, Fabinho, Dembele, Steffen, Pochettino

Ashley Cole Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ashley Cole

Beki wa zamani wa England Ashley Cole, 37, amepewa ofa mpya na klabu ya LA Galaxy - siku chache baada ya kuachiliwa na klabu. (Sun)

Lakini mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea anataka kurejea kwenye kandanda ya Uingereza na amepata ofa kutoka vilabu kadhaa. (Mirror)

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger annegapa kupata nafasi ya ukurugenzi kwa wajibu wake unaokuja baada ya umeneja. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Paris St-Germain watatumia mechi yao na Liverpool kufungua mazungumzo kuhusu kumwendea mlinzi raia wa Brazil Fabinho, 25. (L'Equipe - in French)

Kipa wa PSG Gianluigi Buffon anaamini washambuliaji watatu wa Liverpool - Mohamed Salah, Sadio Mane na Roberto Firmino - ndio bora zaidi dunaini. (Mirror)

Mshambuliaji Mfaransa Ousmane Dembele, 21, amewaambia Barcelona kuwa hataki kuondoka klabuni mwezi Januari. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ousmane Dembele

Manchester City wanakaribia kufikia makubaliano na Columbus Crew na kipa wa Marekani Zack Steffen, 21. (Sky Sports)

Meneja wa Tottenham Mauricio Pochettino anataka kusimamia klabu ya Serie A nchini Italia. (Standard)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anamlenga beki wa Porto mwenye miaka 20 raia wa Brazil Eder Militao. (Daily Record)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Didier Drogba (kulia)

Mshambulji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba, 40, anasema alijifunza sana kutoka kwa mchezaji mwenake wa zamani huko Chelsea na meneja wa Derby Frank Lampard, 40. (Goal)

Barcelona wanataka kubadilisha jina la uwanja wa Nou Camp kwa gharama ya pauni milioni 355. (RAC1)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Damien Duff

Aliyekuwa wing'a wa Chelsea na Jamhuri ya Ireland Damien Duff, 39, yuko kwenye mazungumzo na kocha wa kikosi cha chini ya miaka 20 wa Celtic. (Sun)

Maajenti kutoka vilabu kadhaa wanatarajiwa kuwatazama mabeki wa Wolves Dominic Iorfa, 23, na Ethan Ebanks-Landell, 25, mazoezini. (Birmingham Mail)

Bora zaidi kutoka Jumanne

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anataka kurejea kwenye usimamizi wa kandanda huko Bayern Munich ambao wanamuona Mfaransa huyo kama mrithi wa Nico Kovac. (Telegraph)

AC Milan wamekataa fursa ya kumsaini beki wa Chelsea na England Garry Cahil, 32. (Calciomercato, via Talksport)

Meneja wa AC Milan Gennaro Gattuso hajakana uwezekano wa kumsaini aliyekuwa mshambuliaji wa LA Galaxy Zlatan Ibrahimovic, 37. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Moyes

Mshambualia wa Ubelgiji Eden Hazard, 27, anasema Chelsea wanalenga nafasi nne za kwanza msimu huu na hawatakuwa mabingwa. (Manchester Evening News)

Manchester United wanataka kumsaini mshambuliaji wa West Ham na Austria Marko Arnautovic, 29. (Telegraph)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefufua mikakati zake kumwinda mshambuliaji wa Borussia Dortmund na Ubelgiji Axel Witsel. (ESPN)

Mada zinazohusiana