Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 29.11.2018: Alexis Sanchez, Mousa Dembele, Sousa, Almiron, Callum Hudson-Odoi, Xherdan Shaqiri

Alexis Sanchez Haki miliki ya picha PA

Mshambuliaji wa Chile Alexis Sanchez, 29, anataka sana kuihama Manchester United baada yake kuanza kupuuzwa na meneja Jose Mourinho. (Mirror)

Juventus na Inter Milan wanahusishwa na kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Tottenham na Ubelgiji Mousa Dembele, 31, ambaye mkataba wake katika klabu yake ya sasa utafikia kikomo mwisho wa msimu huu. (Calciomercato)

Newcastle wameongeza juhudi zao za kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay anayechezea Atlanta United Miguel Almiron, 24. (Mail)

Bayern Munich wanapanga kuwasilisha ombi la kumnunua mchezaji anayeng'aa sana akichezea timu ya taifa ya England ya vijana wasiozidi miaka 17 Callum Hudson-Odoi, 18 anayechezea Chelsea kwa sasa mwezi Januari. (Sun)

Haki miliki ya picha SNS
Image caption Moussa Dembele

Southampton wamefanya mazungumzo na Paulo Sousa, meneja wa zamani wa QPR na Leicester kuhusu uwezekano wake wa kuchukua nafasi ya meneja wao wa sasa Mark Hughes ambaye mambo yanamwendea segemnege. (Times)

Huddersfield wanataka wapewe mshambuliaji wa England anayechezea Liverpool Dominic Solanke, 21, kwa mkopo Januari. (Sky Sports)

Meneja wa Everton Marco Silva anataka kumchukua mchezaji wa Watford Abdoulaye Doucoure. Silva alifanya kazi na kiungo huyo wa kati wa Ufaransa mwenye miaka 25 Vicarage Road. (Mirror)

Chelsea wana wasiwasi kwamba huenda jumla ya mashabiki 2,700 wa klabu ya PAOK Salonika wakafika London wakitaka kufuatilia mechi ya klabu yao Europa League Alhamisi bila kuwa na tiketi za kuingia uwanja wa Stamford Bridge. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Abdoulaye Doucoure

Mswizi anayechezea Liverpool Xherdan Shaqiri, 27, amesema ana furaha kuendelea kukaa katika klabu hiyo lakini hajafutilia mbali uwezekano wake kurejea Italia, ambapo aliwahi kuichezea Inter Milan kwa muda awali. (Gazzetta dello Sport, kupitia Star)

Kiungo wa kati wa Uhispania anayechezea Leicester Vicente Iborra, 30, amehusishwa na kurejea katika klabu ya Sevilla Januari, lakini mpango wake wa kurejea una vizingiti tele, kwa mujibu wa mkurugenzi wao wa michezo Joaquin Caparros. (Leicester Mercury)

Beki wa England anayechezea Everton Brendan Galloway, 22, anatarajia kuwa sawa kucheza mwezi ujao baada yake kupata jeraha la misuli ya paja. Kusudi lake kuu ni kupata nafasi ya kuhamia klabu nyingine Januari. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Xherdan Shaqiri

Mkabaji wa zamani wa Newcastle David Edgar, 31, ambaye karibuni zaidi aliichezea Ottawa katika taifa lake la kuzaliwa la Canada, anadaiwa kukaribia sana kujiunga na mahasimu wa Newcastle upande wa kaskazini mashariki, Sunderland. (Chronicle)

Kipa wa Burnley Joe Hart, 31, anasema bado hatafuta kabisa matumaini ya kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya England. (Goalkeepers' Union podcast)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Joe Hart

Leeds wanatafakari uwezekano wao wa kumnunua kipa wa England anayechezea Newcastle Freddie Woodman, 21, mwezi Januari ili kutoa ushindani kwa kipa wao kutoka Ireland Kaskazini Bailey Peacock-Farrell, 22. (Sun)

Bora kutoka Jumatano

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ashley Cole

Beki wa zamani wa England Ashley Cole, 37, amepewa ofa mpya na klabu ya LA Galaxy - siku chache baada ya kuachiliwa na klabu. (Sun)

Lakini mlinzi huyo wa zamani wa Arsenal na Chelsea anataka kurejea kwenye kandanda ya Uingereza na amepata ofa kutoka vilabu kadhaa. (Mirror)

Aliyekuwa meneja wa Arsenal Arsene Wenger annegapa kupata nafasi ya ukurugenzi kwa wajibu wake unaokuja baada ya umeneja. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Arsene Wenger

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho anamlenga beki wa Porto mwenye miaka 20 raia wa Brazil Eder Militao. (Daily Record)

Mshambuliaji wa zamani wa Ivory Coast Didier Drogba, 40, anasema alijifunza sana kutoka kwa mchezaji mwenake wa zamani huko Chelsea na meneja wa Derby Frank Lampard, 40. (Goal)

Barcelona wanataka kubadilisha jina la uwanja wa Nou Camp kwa gharama ya pauni milioni 355. (RAC1)

Mada zinazohusiana