Tetesi za soka Jumanne 04.12.2018: Pulisic, Diaz, Ramsey, Loftus-Cheek, Hernandez, Fabregas

Christian Pulisic Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Christian Pulisic, winga wa Borussia Dortmund

Chelsea kwa mara ya kwanza imewasiliana rasmi na Borussia Dortmund kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili winga wa Marekani Christian Pulisic, lakini huenda klabu hiyo ya Ujerumai ikaitisha euro milioni 70 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye miaka 20 ambaye anapania kujiunga na klabu ya Liverpool. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz, 19, anajiandaa kuondoka Manchester City na kujiunga na Real Madrid, licha ya ombi la Pep Guardiola la kumtaka asalie katika klabu hiyot. (Sun)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anasema kuimarika kwa kiwango cha Aaron Ramsey ni jambo jema kwa kiungo huyo wa Wales wa na kwamba uamuzi wa klabu hiyo ni kutoweka wazi kandarasi yake. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images

Vilabu vya Crystal Palace, Bournemouth, West Ham, Newcastle vinavyoshiriki ligi ya primia pamoja na Schalke ya Ujerumani vinapania kumsajili kiungo wa kimataifa Ruben Loftus-Cheek, 22, anayechezea klabu ya Chelsea baada ya kiungo huyo kukiri kuwa hali ni ''ngumu'' kutokana na kutopangwa katika kikosi cha kwanza. (Mirror)

Mshambuliaji wa West Ham na Mexico Javier Hernandez, 30, ana mpango wa kuhama klabu hiyo mwezi ujao. (El Gol Digital, via Talksport)

Kiungo wa kati wa Chelsea Cesc Fabregas anaweza kuondoka bila malipo msimu ujao na pia anaweza kujadili kandarasi nyingine na klabu ya ughaibuni.

Ajenti wa mwenye asili ya Hispania anadaiwa kukutana na AC Milan, ambao wanammezea mate mshambulizi wa zamani wa Manchester United Zlatan Ibrahimovic, 37. (Football Italia, via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption United Zlatan Ibrahimovic,mshambulizi wa zamani wa Manchester na maneja wa sasa wa klabu hiyo Jose Mourinho

Tottenham, Arsenal na Southampton wameungana na Everton kufuatilia kiwango cha kiungo wa kati wa RB Salzburg Hannes Wolf, 19, ambaye amehusishwa na kiungo muhimu wa Spurs Christian Eriksen. (Mirror)

Southampton wanatazamia kumteua meneja wa zamani wa RB Leipzig Ralph Hasenhuttl kuchukua nafasi ya Mark Hughes kabla ya mwisho wa wiki hii. (Telegraph)

Everton inataka kumsajili kiungo wa kati wa Barcelona Andre Gomes kwa mkataba wa kudumu pale dili yake ya mkopo itakapokamilika mwisho wa msimu huu.

Mshambuliaji mahiri wa Colombia James Rodriguez huenda akahama klabu ya Bayern Munich - ambayo amekuwa akiichezea kwa mkopo wa miaka miwili kutoka Real Madrid - endapo hatapata nafasi pale Niko Kovac atakapo pona jeraha la goti. (Marca)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cesar Azpilicueta, kiungo wa kati wa Chelsea na Uhispania

Kiungo wa kati wa Chelsea na Uhispania Cesar Azpilicueta, 29, ameongezwa mshahara wake kutoka uero 120,000 hadi euro 150,000 kwa wiki baada ya kukubali kutia saini kandarasi mpya itakayomuwezesha kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2022. (Goal.com)

Aston Villa wanatarajiwa kumpatia winga wa Ghana Albert Adomah, 30, kandarasi mpya ya muda mrefu. (Football Ghana)

Meneja wa Brighton Chris Hughton yuko tayari kuwachilia wachezaji wa ziada Ezequiel Schelotto, 29, na Markus Suttner, 31, mwezi Januari mwakani wakati dirisha la usajili litakapokuwa wazi.

Tetesi bora ya Jumatatu

Meneja wa klabu ya Manchester United Jose Mourinho amezua zogo lingine kwa kumshambulia kwa maneno makali Paul Pogba.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil, kiungo wa kati wa Arsenal

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, 30, anapigiwa upatu kuhamia klabu ya Inter Milan msimu huu wa joto. (Sun)

Ozil, ambaye aliachwa nje ya kikosi kilichocheza dhidi ya Bournemouth wiki iliyopita alikosa derby ya London kaskazini kutokana na maumivu ya misuli, ilisema Arsenal. (Daily Mail)

Meneja wa Arsenal Unai Emery amekiri ya kwamba hakuwa na uhakika ikiwa Ozil angelihudhuria mechi ya Arsenal dhidi yaTottenham ambapo waliibuka kidedea. (Independent)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii