Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 05.12.2018: Pogba, Hasenhuttl, Gomes, Fabinho, Ibrahimovic

Paul Pogba Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Paul Pogba,kiungo wa kati wa Manchester United

Juventus wanatafakari kuweka dau la kumnunua Paul Pogba,25, kiungo wa kati wa Manchester United na timu ya Taifa ya Ufaransa. (Sun)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amekataa kutoa taarifa ya kikosi chake kitakachominyana na mahasimu wao wa jadi Arsenal usiku wa leo Jumatano. (Mail)

Kiungo wa kati wa Ureno Andre Gomes anayechezea klabu ya Everton kwa mkopo hajaonesha nia ya kutaka kurudi Barcelona.

Everton sasa inapania kutumia uamuzi wa kiungo huyo wa miaka 25 kuimarisha dau lake kwa lengo la kupampatia mkataba wa kudumu. (Times)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Brazil Fabinho, 25, amesema haoni sababu ya kujiunga na Paris St-Germain mwezi Januari mwakani licha tetesi kuwa huenda akahamia klabu hiyo ya Ufaransa. (UOL, via FourFourTwo)

Mshambuliaji wa LA Galaxy na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 37, huenda akarejea AC Milan hivi karibuni bada ya mazungumzo kuhusiana na mpango huo kushika kasi.(Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatan Ibrahimovic

Manchester City huenda ikamnunua winga wa Leeds United Jack Clarke 18, mwezi January. (Sun)

Meneja wa Monaco Thierry Henry anataka kumsajili mshambuliaji wa Italia Stefano Okaka, 29 ambaye hana raha tena ya kusalia Vicarage Road. (Mirror)

Fulham,Crystal Palace na West Ham wanafuatilia mchezo wa mshambuliaji wa Nantes na Argentina Emiliano Sala, 28. (Mirror)

Southampton wanatarajia kukamilisha shughuli ya kumuajiri meneja wao mpya Ralph Hasenhuttl kutoka RB Leipzig kabla ya mechi ya Jumatano dhidi ya Tottenham. (Guardian)

Arsenal ina matumaini ya kuwashinda Bayern Munich na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsajili winga wa Ivory Coast Nicolas Pepe kutoka Lille. (Mercato 365, via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nicolas Pepe,winga wa Ivory Coast

Crystal Palace na Newcastle pia wanamfuatilia kwa karibu mlinzi wa Real Betis na Uhispania Junior Firpo 22.(Sun)

Kiungo wa kati wa zamani wa England na Liverpool Gerrard anasema hatua ya kuongoza Rangers imemsaidia kujiamini zaidi baada ya kustaafu kutoka uwanjani. (Telegraph)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anatafakari mahali hatua yake ya baadae anapojiandaa kwa msimu ujao wa uhamisho mwezi Januari. (Mirror)

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Cesar Azpilicueta, kiungo wa kati wa Chelsea na Uhispania

Tetesi bora ya Jumanne

Kiungo wa kati wa Chelsea na Uhispania Cesar Azpilicueta, 29, ameongezwa mshahara wake kutoka uero 120,000 hadi euro 150,000 kwa wiki baada ya kukubali kutia saini kandarasi mpya itakayomuwezesha kusalia katika klabu hiyo hadi mwaka 2022. (Goal.com)

Aston Villa wanatarajiwa kumpatia winga wa Ghana Albert Adomah, 30, kandarasi mpya ya muda mrefu. (Football Ghana)

Meneja wa Brighton Chris Hughton yuko tayari kumwachilia wachezaji wa ziada Ezequiel Schelotto, 29, na Markus Suttner, 31, mwezi Januari mwakani wakati dirisha la usajili litakapokuwa wazi.

Kiungo wa kati wa Uhispania Brahim Diaz, 19, anajiandaa kuondoka Manchester City na kujiunga na Real Madrid, licha ya ombi la Pep Guardiola la kumtaka asalie katika klabu hiyot. (Sun)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii