Tetesi za Soka Ulaya Ijumaa 07.12.2018: Steffen, Darmian, Valencia, Suarez, Borini, Wilson, De Jong, Bruce

Antonio Valencia Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Antonio Valencia

Beki wa kulia wa Manchester United Antonio Valencia, 33, huenda akajisajiliwa na West Ham msimu ujao. (Sun)

Meneja wa Derby Frank Lampard amethibitisha kuwa Liverpool wanaweza kumchukua mshambuliaji wao wa zamani Harry Wilsoncan, 21, ambaye amekuwa akiichezea Derby kwa mkopo kufikia Januari. (Talksport)

Fulham wanapania kumsajili mlinzi wa Manchester United Matteo Darmian, 29, lakini kiungo huyo anatafakari kurudi nyumbani, kuna tetesi kuwa Inter Milan na Lazio wanammezea mate. (Tuttomercato, via Talksport)

Wolves wanajiandaa kumpatia ofa ya euro milioni 17 winga wa Japan Shoya Nakajima,24, kutoka klabu ya Portimonense ya Ureno. (Daily Mail)

Meneja wa Newcastle boss Rafael Benitez anaazimia kumsajili mshambuliaji wa Atlanta United Miguel Almiron, 24, na huenda kiungo huyo akaichezea Newcastle kwa mkopo hadi mwisho wa msimu huu. (Mirror)

Kiungo wa kati wa Barcelona Denis Suarez, 24, huenda akahama klabu hiyo endapo hatajumuishwa katika kikosi cha kwanza mara kwa mara.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Denis Suarez, kiungo wa kati wa Barcelona

Chelsea na AC Milan ni miongoni mwa vilabu vikubwa vinavyopigiwa upatu kumsajili. (Calciomercato via Daily Star

Newcastle United wanafuatilia mchezo wa mshambuliaji wa zamani wa Sunderland forward Fabio Borini, mwenye umri wa miaka 27.

Kuna tetesi kuwa klabu hiyo huenda ikaweka dau la kumnunua mwezi Januari iwapo mchezaji huyo anataka kuhama AC Milan. (Tuttomercato, via Sunderland Echo)

Danny Rose amesema heshima ya kucheza katika uga wa Wembley haipo tena baada ya Tottenham kurekodi idadi ndogo ya mashabiki waliyokuja kushangilia mechi yao dhidi ya southampton siku ya Jumatano. (Evening Standard)

Kiungo wa Ajax, Frenkie de Jong, 21, ambaye anapigiwa upatu kujiunga na Manchester City, amekataa kuthibitisha tetesi kuwa huenda akahama klabu hiyo msimu huu wa joto. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Frenkie de Jong mchezaji wa Ajax,

Jack Grealish,23, anayechezea Aston Villa, amesema "hainisumbui kabisa" alipogusiwa pendekezo la kuhamia Tottenham msimu ujao. (Sky Sports)

Mpango wa Rangers kusalia na mlinzi Joe Worrall kwa mkopo zimepigwa zitafaulu baada ya meneja wa Nottingham Forest boss Aitor Karanka kuthibitisha kuwa hamchukua hadi pale mchezaji huyo atakapotoa ombi la kururidi nyumbani. (Daily Record)

Mlinzi wa Juventus Alex Sandro, ambaye amehusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United mwezi Januari mwakani, yuko karibu kuafikiana kwa mkataba mwingine na mabigwa hao wa ligi ya Italia. (Goal)

Kiungo wa kati wa Manchester United Jesse Lingard amethibitisha jinsi walivyopata uchovu baada ya kuiwakilisha Englanda katika michuano ya kombe la dunia. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lingard anasema ushirikiano wake na Romelu Lukaku umemsaidia kufunga magoli msimu huu

Tetesi bora ya Alhamisi

Wolves wanapania kumsajili winga wa Japan Shoya Nakajima kutoka Portimonense ya Ureno mwezi Januari, huku Leicester na Southampton nao wakimmezea mate winga huyo wa miaka 24. (Mail)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anatafakari uhamisho wa mshambuliaji Wesley Moraes kwa kima cha euro milioni 15, japo Fiorentina na Valencia pia zinamfuatilia kiungo huyo wa Brazil . (Sun)

Mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe anasema Frenkie de Jong, 21, ambaye ni kiungo wa kati wa klabu ya Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi atakaribishwa kwa mikono miwiliPSG. (France Football)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii