Kevin de Bruyne wa Man City akana madai ya Guardiola kuwa alikuwa amechoka

Kevin de Bruyne sits on the turf after his injury Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo wa kati wa Manchester City Kevin de Bruyne anasisitiza kuwa hakuchoka mwisho wa msimu uliopita licha ya wasi wasi kutoka kwa meneja Pep Guardiola.

Mbelgiji huyo mwenye miaka 27 amewekwa kwenye kikosi cha kuanza mechi mara mbili pekee katika mechi ambazo mabingwa hao wa Ligi ya Premia wamecheza msimu huu baada ya kupata jeraha.

Guardiola alisema wiki iliyopita kuwa mchezaji huyo alianza msimu akiwa amechoka kufuati mechi za kombe la dunia nchini Urusi.

Lakini De Bruyne anasema alihisi sawa kurudi baada ya msimu wa joto.

Guardiola alihisi kuwa De Bruyne kwamba alicheza mechi 52 kwa miezi 12 kwenye mashindano yote kwa City, na pia kuwa kiungo muhimu kwa Ubelgiji wakati wa Kombe la Dunia kulimwathiri.

"Kevin alimaliza msimu uliopita akiwa amechoka," alisema Guardiola.

"Ulikuwa wakati mgumu kwake na aliporudi nilihisi kuwa alikuwa amechoka kidogo."

Lakini De Bruyne alijibu leo Jumanne kabla ya mechi ya Kombe la EFL dhidi wa Leicester:

Haki miliki ya picha Getty Images

"Sikuwa nimechoka," alisema. "Nilipumzika kwa karibu wiki tatu baada ya miezi 12 ya kucheza. Hicho ni kipindi kifupi? Ndio lakini nilihisi nilikuwa sawa kurudi kucheza.

Jeraha la pili la De Bruyne lilitokea wakati wa mechi ya EFL dhidi ya Fulham Novemba mosi, baada tu yake kurejea kutoka kuuguza jeraha jingine.

"Kawaida kuna wakati katika maisha ya uchezaji ya mchezaji ambapo utajihisi kuchoka lakini nilijihisi sawa. Ni aibu kwamba niliporejea baada ya wiki moja tu, nikaumia na kuwa kwamba siwezi kucheza tena kwa miezi miwili unusu."

"Nilifurahia kurejea na nilitia bidii sana lakini baada ya mechi tatu, ikatokea tena."

Mada zinazohusiana